KATIBU WA ITIKADI,SIASA,HABARI NA UENEZI KATA YA IKWIRIRI AFANYA ZIARA YA UKAGUZI MAJENGO MAPYA YA AFYA.

Katibu Wa Itikadi, Siasa, Habari Na Uenezi kata ya Ikwiriri, Ndg. Yahya Mege Mombokayene  Jana  Mach 21, 2018 Akiongozana Na Kamati Ya Siasa ya Kata Pamoja na Watendaji Wa Serikali wamefanya ziara ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Ccm,Ilitembelea Kituo Cha Afya Ikwiriri na Kukagua Ujuenzi wa Majengo Mapya Matano (5) yatakayo Ghalim kiasi cha Sh Milion 278.

Akizungumza na RAPWINEWS Ndg.Mombokeye Alisema, 

"Tumetembelea katika Kituo cha Afya ilikujirithisha kwa kile kinacho endelea kwa sababu Serikali imetenga Sh Milioni 400 kwa ajiri ya Ujenzi wa Majengo mapya katika Kituo cha Afya Ikwiriri,  na ukizingatia hii ni Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayo ongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameweza kuzielekeza Fedha hizo katika Kituo cha Afya ili kupunguza Kero na Uaba wa Majengo katika Kituo,Ukizingatia sasaivi Ikwiriri ni Mji Mkubwa kwaiyo Idadi ya watu imekuwa kubwa pia"

"Majengo ambayo yameongezeka pamoja na Hodi ya Wazazi,Hodi ya Watoto,Jengo la Kufulia,Jengo la Mtumishi,pamoja na Jengo la Kisasa la Kuhifadhia Maiti,Katika Milioni 300 ambayo imetengwa Katika Vifaa Tiba katika Kituo cha Afya, pamoja na Jengo la (O.P.D)  Alisema Ndg. Mombokeye. 
Mombokeye pia amezungumzia Uhaba wa Madaktali kwenye Kituo iko cha Afya Alisema.  

"Pamoja na hayo kuna changamoto katika kituo cha Afya cha Ikwiriri moja ya changamoto hizi tumezipata toka kwa Mganga Mkuu Mfawidhi wa kitu, Uhaba wa Madaktali, Madaktali wamekuwa wachache ukilinganisha na Idadi kubwa ya watu wanaopokelewa kwa siku wanao hitaji huduma" Alisema Ndg. Mombokeye 

Pia Mombokeye alitoa wito kwa Serikali ya kata namna ngani ya kujipanga na kubuni ili kuakikisha kila kijiji kinapata Zahanati. 
Ndg.Mombokeye halihitimisha kwa kusema "Haya ni Matokeo Chanya, Leadership Is Not About Size Its Wisdom,Tumepewa Jukumu la Kuisimamia Serikali ili Kuondoa Kero na Shida za Wananch Wetu"

Maoni