KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE (shikamoo Parachichi). AWATULIZA MADEREVA BAJAJI- MAKAMBAKO.

Katibu Mwenez wa ccm mkoa Wa Njombe Erasto Ngole ,katika kutambua juhudi za katibu wa Uvccm Wilaya ya Njombe amehudhulia kikao hicho na kuongeza nguvu katika kikao kilicho kuwa  kikisubiliwa kwa hamu kubwa na vijana hao ili kuweza kufufua matumaini yao kwa imani waliojiwekea kwa viongozi wa ccm, kikao kilisimama kwa muda baada ya kuwasili kwa kiongozi huyoo vijana wakionekana kuwa na furaha na kuimba baba...... Baba..... Baba.... Baba.... Baba....... wakizidi kuonesha matumaini yao kwa namna ambavyo viongozi walizidi kuwasili na kukiri kuwa wamethaminiwa na CCM ,wamepaza sauti wakisema Bajaji ni kazi kama kazi Nyingine. 

Kikao hicho kilionekana kupata nguvu kwa uzito wa viongozi waliowasili wakiongozwa na katibu Mwenez wa mkoa, katibu Mwenez wa wilaya Hitler msola, Katibu Hamasa na Chipukizi  Uvccm Mkoa  Jonson Mgimba,Rozana Tewele na Mratibu wa shughuli nzima Katibu wa Uvccm wilaya ya Njombe Ndugu Daniel Muhaza. 

Kwa kutambua yeye ni mtumishi wa watu na amepewa dhamana ya kuwaongoza na kuwatetea watu aliwaacha vijana watoe ya moyoni waliyo nayo ,ambapo wamemuomba kuungana na katibu wa vijana W ya Njombe kutatua kero zao :

-ubovu wa barabara ambayo wanaitumia kwani imekuwa sio rafiki kwa kupitisha bajaji. 

-TRA kuwa na mfumo usio rafiki kwa ulipaji wa mapato Kwa wamiliki wa bajaji hizo. 

-Mzee Adam ni tatizo kwa vijana ambao wanafanya kazi hiyo kwani amekuwa akiwasumbua vijana kwa kuwalipisha fine isiyo na utaratibu unaoeleweka. 

-Pia kutokuwa na utetez kwenye ajira yao Kwan bajaji ni Kazi kama kazi nyingine. 

Mtu wa watu hakuwa Bubu, aliwasihi kuwa watulivu amewasikia na anatambua mchango wao katika jamii wa usafirishaji wa wananchi  hivyo hawatakiwi kubezwa, amewaomba kuungana na katibu wa Uvccm Wilaya ya Njombe na yeye kwa nafasi yake anao mchango mkubwa wa kuweza kuhangaika na hizi kero,pia anatambua kuwa wanalipa ushuru kwa serikali.

Pia amefurahishwa namna ambavyo katibu wa vijana wilaya ya Njombe anavyopambana kutafta maslahi ya vijana wake na kumtaka kutokukata tamaa na kuendelea na moyo huo na kutaka wengine waige mfano huo. 

 Pia amemuagiza katibu Mwenez wa ccm Wilaya ya Njombe kumpiga marufuku mzee adamu kuvaa Nguzo Za CCM pindi anapofanya kazi yake ya kuwatoza fine bajaji na kumtaka ajitathimini je kazi yake hiyo inatenda haki au ni kwa maslahi yake.

Awaomba kuwa watulivu kwani viongoz wa CCM ni wasikivu na watayafanyia kazi malalamiko hayo. 

Imetolewa na Titho stambuli Mtokoma na Erasto k Kizumbe  kutoka ofisi Ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe.

Maoni