KATIBU WA UVCCM WILAYA YA NJOMBE ASAFIRI KM 35, KUWAFIKIA UVCCM  NA KUWAJENGEA UWEZO WA MIPANGO NA UCHUMI ILI KUIPA NGUVU UVCCM -NJOMBE. 

Kiongozi huyo aliyeonekana kutawala vichwa vya habari wiki kadhaa zilizopita baada ya kuwapatanisha SUMATRA na Madereva wa BODABODA, BAJAJI  na HIACE na kujiahakikishia utulivu ndani ya maeneo hayo ameonekana kuwageukia vijana wake nje ya maeneo hayo. 

Ili kuhakikisha anaitendea haki dhamana aliyoibeba ndani ya jumuiya hiyo kusimamia siasa ya vijana kwa manufaa ya ccm na Maisha yetu ya kila siku, ameonekana kubuni mipango ya kuupa nguvu umoja huo na kuipeleka moja kwa moja kwa vijana wake.
Amesafiri mpaka kata za lugenge, utalingolo na luponde kuwafunda vijana hao namna ambavyo wanaweza kubuni miradi ya uvccm ndani ya Kata hizo ili kupata fedha zitakazo weza kuwapa nguvu ya kiutendaji.

 Baada ya kuwasili ndani ya maeneo hayo vijana wameonekana kumpa tano na hongera kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na anaendelea kuifanya ndani ya wilaya yake. 

Katibu huyo aliyeonyesha kipaji cha pekee cha kufundisha ubunifu, na usimamizi wa miradi.

Ametoa maelekezo kwa uvccm kuweza kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kujisimamia katika kuhakikisha wanapanga budget ya mwaka mzima ya kiutendaji ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa, lakini ili kuweza kufanikisha zoezi hilo ni lazima waongeze ubunifu wa kutafuta fedha kwa kubuni miradi ndani ya Kata zao, 
Uwezo wake wa haraka wa kujifunza mazingira ameonekana kuzitambua fursa vyema zilizopo ndani ya wilaya yake amewakumbusha kutumia fursa zinazowazunguka ndani ya kata zao ,ametolea mfano kilimo cha parachichi, viazi,miti na maua wanaweza kufanya kwaajili ya manufaa ya jumuiya hiyo na maisha yetu ya kila siku. 

Kwa pamoja viongozi wa jumuiya Hiyo wameoneka kufurahishwa namna ambavyo katibu wao amekuwa akipasua anga kwa maslahi ya vijana, wasema wako pamoja nayeye na wako tayar kumpa ushirikiano kwa kila jambo ndani ya umoja huo. 

Wanampongeza kwa kazi nzuri na wanajivunia kwa katibu huyo kuwa na mahusiano mazuri kwa vijana na kutuliza mizuka ya vijana walipoteza mwelekeo. 

Nasisi pia wahabarishaji tunakupongeza katibu wa uvccm wilaya ya Njombe Ndugu -Daniel Muhaza ......habari zako tunazihabarisha. 

Kazi yetu ni ndogo, ila habar hii ni kubwa. 
  
Nguvu ya habari inapewa nguvu na Ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe. (Titho stambuli Mtokoma na Erasto kizumbe).

Maoni