KATIBU WA WAZAZI MKOA WA NJOMBE AFANYA ZIARA YA KUHAKIKISHA ANAIMARISHA MIRADI YA JUMUIYA  NA SHULE ZA WAZAZI ZINAKUWA NA KIWANGO BORA CHA ELIMU  MKOANI NJOMBE

Jumuiya ya wazazi mkoa wa Njombe yajipima upya juu ya uimarishaji miradi ya jumuiya hiyo na utoaji wa elimu, kupitia kitengo chake cha mazingira, elimu na malezi, ili kuweza kuifanya jumuiya hiyo kuwa na nguvu kwani anaamini siasa bila uchumi haiwez kwenda na wao kama wazazi wanawajibu wa kusimamia malezi na elimu kwa jamii. 

Ziara iliyofanywa na mtendaji wa jumuiya hiyo ngazi ya Mkoa ndugu Lucas Nyanda imeonekana kuwa na mipango na mikakati ya kuboresha na kubuni na kufufua miradi ya jumuiya hiyo.

Katibu huyo ambaye  ameonekana kuwa na mikakati na mipango mikubwa ya jumuiya hiyo katika kuhakikisha inakuwa na uchumi imara ambapo ameweza kutoa semina elekezi kwa wasaidizi wake alipofanya ziara katika wilaya zake mkoani Njombe, ambapo amefanya ziara wilaya ya ludewa.

Uzoefu na uwezo alionao katibu huyo ameonekana kuwafunda vyema watendaji na wasaidizi Wake ambao wamekuwa wanamsaidia shughuli za jumuiya hiyo. 

Ziara hiyo ambayo imeonekana kuwa na matunda ndani ya jumuiya hiyo amefanikiwa kuunda bodi ya shule ya secondary ludewa baada ya bodi ya zamani kumaliza muda wake, Baada ya kupata bodi mpya ameiomba bodi hiyo kuleta mabadiliko chanya ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazo ikabili Shule,amewaomba wajumbe kubuni mipango itakayoisaidia shule hiyo kusonga mbele, sambamba na ustawi wa uchumi wa shule hiyo. 

Baada ya kuzungumza na wajumbe wa shule hiyo amepanda wa parachichi kama kuacha alama baada ya kukamilisha zoezi hilo. 

Mara baada ya kupatikana kwa bodi hiyo mpya, wajumbe walifanikiwa kuchangia vitanda viwili, Magodoro mawili na pesa taslimu Shillingi  200,000/=.

Pia wajumbe wa Bodi wameweza kuahidi maliza changamoto zinazoikabili shule hiyo kwa kufanya harambee inatarajia kufanyika mapema mwa mwezi wa nne. 

Akiwa wilayani humo alifika shule ya secondary masimbwe ambapo alikutana na Bodi ya shule ya secondary masimbwe kwa lengo la kuona maendeleo yake tangu ichaguliwe mwaka jana Ndugu Lucas Nyanda ameonekana kuridhishwa na mipango yao ya kuiwezesha shule, ameweza kuwapongeza kwa kuweza kuomba wadau kutoka nje ya nchi kuja kusaidia shule hiyo kwa lengo la kusaidiwa kujengewa mabweni na uanzishwaji wa ufugaji wa kuku kama Mradi shuleni hapo. Amewaomba kuzidi kujiimarisha zaidi katika usimamizi wa maendeleo ya shule hiyo. 

Pia amemshukuru mwkt wake wa mkoa Ndugu Josephat Mpogolo kwa kuzidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika kusimamia maendeleo ya jumuiya hiyo.
 
Katika majumuisho yake aliwaomba maeneo yote ya shule kuyapanda miti ya biashara kama maparachichi na korosho kwa shule ya ludewa secondary.

Imetolewa na Titho stambuli Mtokoma na Erasto kizumbe kutoka ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe.

Maoni