KUNDI LINALOJIITA "WAKOREA" LAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA UHALIFU MJINI MBEYA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu maarufu kama "Wakorea".

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya Operesheni maalum pamoja na misako katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya. Operesheni hii ililenga kukamata wahalifu mbalimbali likiwemo kundi la vijana wanaojiita "Wakorea" ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Operesheni hii imefanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambayo ni Ivumwe, Mwakibete, Mwambene, Mama John, Ilomba, Mafiati, Makunguru, Iyela na Isyesye.

Katika Operesheni hii maalum, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita kwa  tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu. Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-

KELVIN RAPHAEL [22] Mwakibete Bomba mbili ambaye ndiye kiongozi wa kundi hili la uhalifu @ Wakorea.

CLEMENCE CHRISTOPHER @ MWAKALINGA [23] Mkazi wa Mwakibete Viwandani.

CHARLES MWASUMBI [21] Mkazi wa Mwakibete

EDGA EDWARD [20] Makondeko Mwakibete

IPYANS NDUNGURU [21] Mkazi wa Mwakibete

ADEN MWALUKASA [35] Mkazi wa Mwakibete

Pia katika Operesheni hii maalum ya kuwasaka vijana wanaojihusisha na uhalifu hapa Jijini Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana watatu [03] kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji nyakati za usiku na mchana. Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-

GODFREY JOSEPH @ MHENGA [20] Mkazi wa Ilemi Mapelele

GODFREY PAUL @ MWAKASAJE [39] Mkazi wa Ilemi Mapelele

MTEMI YAHAYA @ MWASANGA [42] Mkazi wa Uyole

Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa walikutwa na vifaa mbalimbali walivyokuwa wakivitumia kuvunjia ambavyo ni:-

Bisibisi – 03

Nyundo – 01

Mkasi – 01

Aidha watuhumiwa hao walikutwa na mali mbalimbali za wizi:-

Flat Screen aina ya Home base

Flat Screen aina ya Samsung

TV ya kawaida aina ya Home base

Sub Woofer 01

Deck 03 aina ya Singsung 02 na Fusion 01.

Aidha mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane [08] kutokana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao walifikishwa Mahakamani na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje.

Pia watuhumiwa kumi na mbili [12] ambao walikamatwa hivi karibuni katika Operesheni/Misako iliyofanyika huko katika maeneo ya Ilemi, Juhudi, Makunguru na Mwenge hapa Jijini Mbeya ambao kesi zao zinaendelea katika Mahakama ya Mwanzo Iyunga

Watuhumiwa wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya Upelelezi kukamilika.

WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipati kipato. Aidha anatoa onyo kali wafanyabiashara ya vilezi kufuata sheria na taratibu za biashara yao ikiwa ni pamoja na kufungua na kufunga sehemu zao za biashara muda sahihi kwa mujibu wa sheria.

Maoni