Lema Afunguka Haya Baada ya Polisi Kusema Bado Aijafahamika Risasi Iliyomuua Akwilina


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameongea kuhusu taarifa iliyotolewa na Kamanda wa kanda maalum ya DSM Lazaro Mambosasa kuhusu silaha iliyotumika kumuua Akwilina kuwa bado haijajulikana na wanaendelea na upelelezi.

Lema kupitia akaunti yake ya Twitter ameandikia kuwa ameitafakari kauli ya Mambosasa kuhusu tukio la Akwilina juu ya silaha iliyotumika.

“Nimeitafakari kauli ya Mambosasa inayohusu tukio la Akwilini kuhusu silaha iliyotumika, bila shaka kuna dhambi kubwa inapangwa nawasihi Wana CHADEMA kuwa makini wakati huu kwani si ajabu ukasikia kuwa Ile silaha iliyotumika kumuua Akwilini imekutwa nyumbani kwa Kiongozi wa CHADEMA” -Lema

Godbless E.J. Lema@godbless_lema

Nimeitafakari kauli ya Mambosasa inayohusu tukio la Akwilini kuhusu silaha iliyotumika,bila shaka kuna dhambi kubwa inapangwa nawasihi WanaChadema kuwa makini wakati huu kwani si ajabu ukasikia kuwa Ile silaha iliyotumika kumuua Akwilini imekutwa nyumbani kwa Kiongozi wa CHADEMA.

Maoni