MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE: MKALIPA AWAASA VIJANA KUWAHESHIMU NA KUWALINDA WAKINA MAMA

Na Shabani Rapwi.

Alhamisi 8 March 2018.

Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. NASRI MKALIPA amewatakia kheri wanawake wa Kata ya Chamazi na  dunia nzima  sambamba na kuwaasa vijana kuwaheshimu wazazi hao.

Salaaam hizo amezitoa leo Alhamisi 8 March 2018 wakati akizungumza na mtandao wa RAPWI NEWS kutoka moja kwa moja kwenye ukumbi yalipofanyika  maadhimisho hayo ambayo kwa Mkoa wa Dar es Salaaam yamefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City uliopo Ubungo, Dar es Salaam.

"Nikiwa kama kiongozi wa Vijana wanawake kwa wanaume, vile vile kama kijana ninayejua uchungu wa mama napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia kheri ya maadhimisho ya siku ya wanawake, wanawake wote wa Kata ya Chamazi, Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania na Duniani kwa ujumla, Mungu awape afya njema na baraka, wawe na kauli thabiti, wafanya kazi kwa bidii sambamba na kumuombea Rais wetu Mh. John Pombe Magufuli" alisema Mkalipa.

Pia Ndg. Mkalipa aliwata vijana wa Kata ya Chamazi na Kata zingine zote kuwa na heshima kwa mama zao kwani wamepata tabu sana juu yao.

"Mama zetu wamepata tabu tangu tupo tumboni, wakatulea kwa shida na mpaka sasa tumekuwa wakubwa, napenda kutumia nafasi hii kuwaasa vijana wenzangu kuwalinda, kuwaheshimu na kuwatunza mama zetu daima milele" alisema Mkalipa.

Maoni