MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA YATOA ONYO KALI KWA MATAPELI WA BIMA.

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imetoa onyo kali kwa watu wanaowatapeli wananchi kwa kuwauzia bima za kugushi na hivyo kuwasababishia hasara na kuikosesha Serikali mapato,Matapeli hao ambao wengi wao hawana leseni za kufanya biashara ya Bima wametakiwa kuacha mara moja wizi huo kwani mkono wa sheria unawasaka ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza wakati wa zoezi la ukaguzi wa bima katika Vyombo vya moto lililofanyika Mjini Dodoma ,Bibi Stella Guli Rutaguza amesema jumla ya magari 586 yalifanyiwa ukaguzi, ambapo  wamebaini  magari 25, pikipiki za miguu mitatu 5(bajaj) pikipiki za miguu miwili 2 yakiwa na Bima za kugushi huku magari mengine 19 yakiwa hayana bima.

 Rutaguza amesema kuwa wamefaminikiwa kuwakamata watu Wawili ambao wanatuhumiwa kujihusisha na kuuza bima za kugushi kwa wananchi na tayari wako mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

Bibi Stella Rutaguza amesema zoezi la kuwasaka watu wanaouza bima feki kwa na kuwaibia wananchi na Serikali ni endelevu hapa Dodoma na Nchi nzima kwa ujumla.

"Tunataka kukomesha tabia hii chafu kwenye Soko la Bima", hivyo tunawataka vishoka wa Bima popote walipo watafute kazi halali ya kufanya maana Mamlaka ya Usimamizi wa Bima haitawafumbia macho na mkono wa sheria hawataukwepa", alisema Rutaguza.

Amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kutokuibiwa na matapeli hawa wa Bima kwa kununua Bima kwenye ofisi zilizosajiliwa na kupewa Leseni na Serikali kwa ajili ya kufanya biashara ya Bima na kuacha kununua Bima kiholela mitaani kwa watu wasiofahamika.


Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima(TIRA) Kanda ya Kati Bi.Stella Rutaguza.Picha na Vero Ignatus Blog.

Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA)  kanda ya kati ,Adamu Maneno (katikati)akihakiki stika ya bima kama ni halali au feki stendi ya  Hiace jamatini Dodoma,kulia kwake ni PC Majenga,kushoto kwake ni Liberath wakala wa bima mkoani hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.

Afisa mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Kati Rojas Msagati (katikati)akiwa anahakiki moja ya gari katika stendi ya jamatini Dodoma ,kulia.kwake ni WP 4079CPL Karitas.Picha na Vero Ignatus Blog.

Maoni