Mjumbe Baraza kuu UVCCM Taifa Mkoa Dar es Salaam Ndugu Gwantwa Alex mwakijungu Leo jumapili Tarehe 10 March 2018 amezindua Mfumo wa Kanzi Data (Data Base) kwa shughuli za jumuiya ya vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.
Kazi kubwa ya mfumo huu itakuwa ni upatikanaji wa taarifa muhimu, usajili wa wanachama wapya, Mfumo wa Malipo ya wanachama na Shughuli nyingine mbali mbali.

Hafla hii imefanyika Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Tekelezaji UVCCM Mkoa wa Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa DSM Musa Kilakala, Katibu hamasa Mkoa Saady Khimji, na wenyeviti wa UVCCM wilaya ya Ilala na kigamboni.
Maoni
Chapisha Maoni