MBARAZA UVCCM TAIFA KUPITIA MKOA WA MAGHARIBI ZANZIBAR NDG. KASSIM HASSAN HAJI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UVCCM CHAMAZI

Leo Ijumaaa 2 March 2018

 Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kupitia Mkoa wa Magharibi Zanzibar amekutana na kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa UVCCM wa Kata hiyo Ndg. NASRI MKALIPA na Katibu wa Jumuiya hiyo Ndg. JUMA BEGA ZONZO. 

azungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Kata ya Chamazi iliyopo Chamazi Magengeni.

Lengo la ziara hiyo ni kuzungumza mustakabali mzima wa Jumuiya ya Vijana sambamba na kufahamiana baina ya viongozi kutoka sehemu mbalimbali.

Sambamba na hilo Mbaraza Kassim Haji aliwasifia viongozi wa Kata ya Chamazi kwa ubunifu mkubwa walionao jambo lililopelekea mpaka yeye kuwa na hamu ya kuja kuzungumza nao.

Pia Mbaraza Haji Kassim Haji alikisifia sana kitabu cha hatubebi Mabegi na kuwataka vijana kukisoma kwani kitawasaidia kuwa wajasiri na wa kweli, jambo litakalopelekea Mapinduzi ya kweli ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi.

Imetolewa na
Idara ya Hamasa na Chipukizi.
Kata ya Chamazi.

Maoni