MBARONI KWA KUUA MKEWE KUFICHA MAITI KWENYE MBUYU.

Mtu mmoja kwa jina Benard Shumba mkazi wa Singida anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kumuua mke wake miaka Minane iliyopita kisha kuuficha mwili huo kwenye Mbuyu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ,Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu. 

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki ya mwili wa mwanamke huyo.

Maoni