MD KAYOMBO UBUNGO TUNAJIPAMBANUA KWA KUWA MANISPAA YA TOFAUTI

Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ameyasema hayo leo tarehe 07/03/2018 wakati anakagua vibanda vya wanawake wajasiliamali ambao wanafanya maonyesho ya bidhaa zao kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Maadhimisho hayo kimkoa wa Dar es salaam yanafanyika  Manispaa ya Ubungo katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam yakiambatana na maonyesho ya bidhaa zilizotengenezwa na wanawake wajasiliamali wa mkoa wa Dar es salaam.

Kayombo amefurahishwa na jitihada za wanawake wajasiliamali ambao wanaonyesha bidhaa katika vibanda anuai na akatoa maagizo yafuatayo:

"vikundi vyote vya wanawake wajasiliamali katika manispaa ya Ubungo katika kata zote kumi na nne maafisa maendeleo ya jamii wahakikishe vikundi vimesajiliwa"Alisema Kayombo.

"Vikundi vyote vya wanawake wajasiliamali maafisa maendeo katika kata zote wawaelimishe juu fursa za mikopo inayotolewa na Manispaa kwa kuwa ni mikopo yenye mashariti nafuu hata riba yake ni ndogo" Alisema Kayombo.

"Wanawake wote wajasiliamali wa Manispaa ya Ubungo wajitahidi katika bidhaa zao kuwa na Standard ili kupanua wigo wa masoko ni lazima bidha iwe imepakiwa vizuri, iwe inaonyesha "expired date" na pia "balcon" Alisema Kayombo

Aidha Mkurugenzi Kayombo anawakaribisha wanawake wote wa Mkoa wa Dar es salaam kuhudhuria maonyesho hayo kesho tarehe 8/03/2018 katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam.

Maonyesho hayo yanatoa fursa ya kipekee kwa wanawake kutambua nafasi yao katika jamii na namna wanavyoweza kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa lengo la kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

#Karibuni sana Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo#

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Maoni