MKALIPA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA DC MSTAAFU WA WILAYA ZA ILALA, ARUSHA MJINI, MBEYA MJINI,  NGARA,  NZEGA,  SHINYANGA MJINI,  DODOMA VIJIJINI,  SIKONGE NA SUMBAWANGA MH. EVANS BILAL BALAMA

Na Shabani Rapwi.

Kunduchi, Dar es Salaam.

Katika kuendelea kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu siasa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi Ndg. NASRI MKALIPA amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Wilaya Mstaafu Mh. EVANS BILAL BALAMA.

Mazungumzo hayo  yamefanyika leo Alhamisi 22 March 2018 nyumbani kwa mkuu wa Wilaya huyo Mstaafu Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Wakiwa katika mazungumzo hayo Mkuu wa Wilaya huyo alisisitiza vijana kuwa wakweli, watimizaji na wafatiliaji wa maagizo wanayopewa na viongozi wa juu yao kuyatoa kwa viongozi wa chini yao kwani itasaidia ufanyaji kazi. 

Pia Mh. Balama alimpongeza sana Rais wa awamu ya tano Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kwa ufanyaji kazi uliotukuka sambamba na misimamo aliyonayo.

Sambamba na hilo Mh. Balama alimpongeza sana Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Chamazi Ndg. NASRI MKALIPA kwa utunzi mzuri wa kitabu cha HATUBEBI MABEGI kwani kinamsaidia kijana kuwa na misimamo sambamba na kufanya kazi kwa bidii.

Kabla ya kufunga mazungunzo hayo Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Chamazi Ndg. MKALIPA alimshukuru Sana Mh. Balama sambamba na familia yake kwa mapokezi na nasaha nzuri walizompa pia kwa kununua nakala tano za kitabu cha hatubebi mabegi.

Maoni