Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi, Ndg. NASRI MKALIPA ameshiriki kongamano la K.M.O (Kijana Mwelevu Organization) lililofanyika Jana Machi 17,2018 katika uwanja wa ofisi ya serikali ya Mtaa Rufu iliyopo Rufu Kata ya Chamazi. Lengo kuu la kongamano hilo kubwa ni kumfanya kijana kuwa msikivu,mwenye kutafakali, kuwa tofauti na mwelevu.
Akizungumza na RAPWI NEWS, Ndg. Mkalipa amesema "Vijana ili tuwe na thamani na kuheshimika katika jamii,tunapaswa kuwa wakweli,wathtubutu, wasikivu, waerevu sambamba na kutokuwa waoga,katika maamuzi yenye tija kwenye jamii" alisema Mkalipa. "Hatuna budi kuwasikiliza na kuwaheshimu wakubwa na watoto kwani heshima huleta maelewano na upendo kati yetu" alisema Mkalipa.
"Sisi kama vijana ambao ni viongozi wa leo na kesho hatuna budi kuwasisitiza vijana wenzetu kufanya kazi kwa bidi ili kuendana na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU"
Pia Mkalipa alesema Rais wetu anafanya sana kazi kwa hiyo vijana hatuna budi kumuunga mkono kwa sisi kufanya kazi, kumlinda na kumuombea kwa Mungu. Wakati huo huo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kijichi Ndg. Belton Wambura ambae aliambatana na kikundi hiko alimshukuru Ndg. Mkalipa kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Kata ya Chamazi na Kijichi.
Maoni
Chapisha Maoni