MKURUGENZI ATOA POLE KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA MBAGALA RANGI TATU

 MKURUGENZI wa Halmashauri wa Temeke jijini Dar es Salaam, Nassib Mmbagga ametoa pole kwa wafanyabiashara wa soko la Mbagala Rangi tatu  ambao wamepoteza mali zao baada ya kuungua kwa soko hilo.

Soko hilo ambalo lilikuwa na wafanya biashara zaidi ya 500 lilianza kuteketea usiku wa kumkia leo.

Akizungumza leo,Mkurugenzi  amesema Halmashauri imepanga kukutana na wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katika soko hilo.

Amesema lengo ni  kuangalia ni jinsi gani halmashauri itawasaidia

   Vibanda vilivyokuwa vinamilikiwa na wafanyabiasharawa Soko la Mbagala Rangi Tatuvikiwa vimeteketea kwa moto.

 Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la Tukio.

Maoni