Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amewaua watu 26 mjini Kabul

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amewaua watu 26 mjini Kabul baada ya kujilipua akiwa miongoni mwa kundi kubwa la watu waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya wa Kiajemi.

 Kumekuwa na hali mbaya katika hospitali mkabala na eneo hilo la mlipuko ambako ndugu waliotaharuki walipiga kelele wakati wakikumbatia miili iliyojaa damu ya wapendwa wao, katika kile kilichoonekana hapo kabla kuwa siku ya kawaida ya sherehe kwa familia za Waafghanistan.

 Tawi la kundi la Dola la Kiislamu nchini Afghanistan lilidai kuhusika na mashambulio hayo katika eneo wanaloishi Washia wengi, ikiwa ni shambulio la tano la kujitoa muhanga katika mji mkuu wa Afghanistan katika wiki za hivi karibuni.

 Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Nasrat Rahimi amesema watu wengine 18 wamejeruhiwa katika mlipuko huo. 

Maoni