MWANAFUNZI ATAFUNWA NA MAMBA WAKATI AKIOGELEA ZIWA VICTORIA.

Na Gharos Riwa, Bunda. 

Mtoto aliyejulikana kwa majina ya Raban Benjamin Makasi miaka 11 aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nyabehu katika halmashauri ya mji wa Bunda amezikwa fuvu Lake la kichwa,mifupa pamoja na shati alilokuwa amevaa baada ya kuuawa na mamba katika ziwa Victoria wakati ameenda kuoga.

Tukio hilo limetokea March 25 mwaka huu wilayani Bunda mkoani Mara.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyabehu bwana Richard Kanga amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kwamba taarifa hizo za kukamatwa na mamba mtoto huyo amezipata baada ya mdogo wake kupiga wangwi(yowe) kuomba Msaada ambapo aliamu kufuatilia na baada ya kufika eneo la tukio alishuhudia akiwa pamoja na wananchi wengine mamba huyo akiwa na mtoto Huyo.

Amesema walipoamua kumfuatilia alizama majini na baadae walipoendelea kwa muda mrefu kidogo wakiangaikia kujua Mahalia alipo mamba huyo walikuta ufukwani mwa zaiwa akiwa tayari ameliwa sehem nyingine ya mwili na kubakia fuvu,mifupa na shati alilokuwa amevaa.

Hivi karibuni Afisa wanyamapori wa wilaya ya Bunda Marwa Kitende akiwa katika kijiji cha Tingirima akitoa elimu juu ya uhifadhi na namna ya kudhibiti wanayama hatari alieleza kwamba mnyama akimuua mwananchi analipwa fedha kiasi cha shilingi milioni Moja, na ulemavu wa kudumu ni shilingi laki tano kama pole.

Maoni