Mwanamke Aliyedhalilishwa na Kuteswa Wakati Akijifungua Kulipwa Milion 56

KENYA: Mahakama Kuu imeamuru mwanamke(Josephine Majani) aliyedhalilishwa na kuteswa wakati akijifungua katika hospitali ya umma, alipwe fidia ya takribani Tsh. Milioni 56.5.
-
Mahakama ilidai mamlka ya afya ilikiuka haki za kimsingi za Bi. Majani alipotengwa na kukosa kuhudumiwa mwaka 2013
-
Aliyoyapitia Bi. Majani mikononi mwa wauguzi hao yalipata kujulikana baada ya mtu kurekodi video kwenye simu yake na kuiweka kwenye mtandao wa kijamii
-
Akizungumzia uamuzi huo, Bi Majani amesema amefurahia kwa kuwa hatimaye haki imetendeka na kuwa atatumia fedha hizo kumlea mwanaye

Maoni