MWENDELEZO WA ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM WILAYA YA BUNDA JIMBO LA BUNDA

Ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bunda Ndg Gasper Charles akiambatana na Katiba wa UVCCM Wilaya Ndg Steven E. Shija wameendelea na Ziara leo katika Kata Mbili ambazo ni Hunyari na Mugeta. 

Katika Ziara hiyo Mwenyekiti alikutana na Mabaraza ya UVCCM Kata pamoja na Viongozi wa Chama pia alikabidhi Muhuri, Kanuni na Daftari maalumu kwa ajili ya kuandikia Kumbukumbu Muhimu za Jumuiya. 


Katika Kata ya Mugeta Katika kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya pamoja na Katibu wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe Mganga Jongolo, pamoja na Viongozi wa Jumuiya na Chama walitembelea Kwenye Eneo panapojengwa Kituo Cha Afya ambapo Serikali imetoa Milioni Mia Nne na kubaini Changamoto mbalimbali zinazokwamisha kuanza kwa Ujenzi huo pamoja na uwepo wa Viashiria kutoka kwa Wananchi mpaka sasa Msingi tu ndiyo umechimbwa tangu Fedha zilipofika Mapema Mwezi wa Kwanza


Pia Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya akiwa na Katiba waliongozana na Diwani pamoja na Viongozi wa Jumuiya na Chama kuangalia maendeleo ya Zoezi la Ujenzi wa Madarasa Matatu ambayo Serikali imetoa takribani Milioni Sitini na Sita kwa ajili ya Ujenzi huo

Mwisho Katibu wa UVCCM Wilaya alisisitiza umuhimu wa Kujiunga kwenye Vikundi, na kuvitaka Vikundi vilivyokopeshwa kurejesha Fedha hizo ambapo Afisa maendeleo wa Kata alikuwepo, na Viongozi wote walikumbushwa kufanya Vikao kwa Mujibu wa Kanuni na kuingiza Wanachama wapya kwa Kuzingatia taratibu na Kanuni za Chama na Jumuiya

       TUPO KAZINI


Imetolewa na :-
Ndg S.E.Shija
Katibu wa UVCCM Wilaya
Bunda, 

Maoni