MWENYEKITI UVCCM MKOA WA KUSINI UNGUJA NA KAMATI YAKE YA UTEKELEZAJI WAFANYA ZIARA. 

Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja Nd Latifa Khamis Juakali  Mar 03/03/2018 amekutana na viongozi mbali mbali ngazi ya tawi wadi jimbo kwa lengo la kutoa shukurani kwa kuchaguliwa.

Katika ziara hiyo  Mwenyekiti alipokea maoni ushauri na michango mbali mbali kutoa kwa Kusini


Vijana hao walisema mengi baadhi yao walisema wazi kuwa kuna baadhi ya mashekha ni kikwazo kwao.

Wengine walifika mbali kwa kusema kuwa mfumo wa ajira ndani ya mkoa wa Kusini ni mbovu kwa maana hata vijana wa CCM walisoma wapo ila hawaajiriwi.

Baadhi ya vijana wamesema kuwa kuna kazi za chama zinatekelezwa bila ya wao kushirikishwa wakati wao ni viongozi halali katika maeneo husika.

Wapo pia waliosema ahadi zisizo telekezeka kutoka kwa viongozi wa chama madiwani wabunge na wawakilishi ni sehemu ambayo inawapoteza vijana

Mwisho vijana walisema jografia ya Wilaya ya kati ni ngumu sana na kwa hiyo viongozi wanaomba wapaitie usafiri japo baskeli ili wawafikie wanachama wao.

Baada ya Maoni na wanachama kutoa changamoto zao za maeneo yao Mwenyekiti aliruhusu wajumbe alio ongozana nao watowe majibu kwa kina kwa yale ambao yapo ndani ya uwezo wao

Mwenyekiti nae alitoa ufafanuzi kwa yale yote yaliyowasilishwa hatie alitoa shukurani kwa wajumbe waliohudhuria na kuchangia kwa uwazi bila ya woga.

Mwenyekiti aliwashauri vijana wasiache kusema mema na mazuri yaliyofanywa na serekali ya CCM kwa maana yapo mengi mazuri yanafanywa kila siku

Ziara hiyo ya Mwenyekiti na wajumbe wake wa kamati ya utekelezaji itaendelea tena 04/03/2018 amvi Wilaya ya Kusini.

Imetolewa na:
ALAWI HAIDAR FOUM.
KATIBU UVCCM MKOA WA KUSINI UNGUJA.

Maoni