MWENYEKITI UVCCM  MKOA WA RUKWA AFUNGA LIGI YA KATA, WILAYANI SUMBAWANGA MJINI AKABIDHI JEZI,FILIMBI,FEDHA NA MIPIRA YA MIGUU

Na- Gaston Wakulyamba

Mwenyekiti Wa Vijana Wa Mkoa Wa Rukwa Ndg Ramadhani Shabani Akiongozana Na Katibu Hamasa Na Chipukizi Ndugu Andrea Matanila,Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM Taifa Ndugu Emmy Mwasile Mjumbe Kamati Ya Utekelezaji Buttoh Lubusi Pamoja Na Mwenyekiti Wa Vyuo Na Vyuo Vikuu Mkoa Ndugu Hassan Nguta. 

Jana Amefunga Ligi Ya Mpira Wa Miguu Katika Kata Ya Malangali Ambayo Ilikuwa Chini Ya Udhamini Wa Jumuiya Hiyo Ya Vijana Chini Ya Usimamizi Wa Uongozi Wa Vijana Wa Na Mwenyekiti Wake Donald Mwanawima Wa Kata Hiyo.

Akifunga Ligi Hiyo Ya Mpira Wa Miguu Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Alitumia Fursa Hiyo Kuwapongeza Vijana Hao Wa Kata Hiyo Kwa Kuona Umuhimu Zaidi Wa Kuthamini Michezo Kwani Kupitia Michezo Zipo Faida Nyingi Mno Kama Kijana Unaweza Kuzipata Na Haswa Ktk Kukuza Vipaji Vya Wachezaji Ktk Mkoa Wetu Lakini Kama Haitoshi Hata Kuimarisha Afya Zetu Hivyo Nitumie Fursa Hii Kuwapongeza Sana Vijana Wenzangu.Lakini Pia Niwapongeze Sana Viongozi Wa Jumuiya Ya Vijana Kata Kwa Kazi Kubwa Mnayoifanya Katika Kuwaonganisha Vijana Kwani Haya Ndio Mambo Ambayo Vijana Wanataka Kuyaona.Nami Nawaambia Vijana Wenzangu Mambo Mazuri Yapo CCM Hivyo Msihadaike Na Wengine Wanaowapotezea Muda Kwa Kuwafanya Muandamane Hivyo Bila Sababu Za Msingi Huku Wakiwa Wamelenga Kunufaika Wao Na Familia Zao.

Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Alitumia Fursa Hiyo Kuwasisitiza Vijana Hao Kujiunga Ktk Vikundi Vya Ujasiliamali Kwani UVCCM Mkoa Wa Rukwa Imejipanga Vyema Kuhakikisha Vijana Hao Wananufaika Na Mkopo Kutokana Na Asilimia Tano Ya Mapato Ya Ndani Ambapo Kwa Halmashauri Ya Sumbawanga Mjini Imetengwa 50 Milioni Kwa Ajili Ya Vijana.Lakini Pia Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Pia Alitumia Fursa Hiyo Kuwakumbusha Wenyeviti Wa Vijiji,Mitaa Na Vitongoji Kuwasomea Mapato Na Matumizi Wananchi Wao Kwani Hiyo Haipaswi Kuwa Agenda Ambayo Itainyima Kura CCM Ktk Uchaguzi Ujao Wa Serikali Za Mitaa 2019.

Akimalizia Kuzungumza Mwenyekiti Huyo Alisema Nitumie Fursa Hii Kuwapongeza Timu Zote Mlizoshiriki Ktk Ligi Hii Lakini Jumuiya Ya Vijana Tunaahidi Kuboresha Zaidi Ligi Ijayo Kwani Tutaongeza Mipira Miwili Na Jezi Seti Moja Tena.


UVCCM MPYA KWA MASLAHI MAPANA YA VIJANA WA RUKWA.

Imetolewa Na

Katibu Hamasa Na Chipukizi

Andrea Matanila

Maoni