MWENYEKITI UVCCM MKOA WA RUKWA NDG RAMADHANI SHABANI AFANYA ZIARA KATA YA MSUA SUMBAWANGA MJINI,AGAWA KADI 104, ATOA MIPIRA MIWILI NA FILIMBI DOZEN MOJA KWA TIMU ZA KATA HIYO

Mwenyekiti Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Ndg. Ramadhani Shabani Akiongozana Na Katibu Hamasa Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Ndg. Andrea Matanila Pamoja Na Mwenyekiti Wa Vyuo Na Vyuo Vikuu Mkoa Wa Rukwa Ndg Hassan Nguta Pamoja Na Mjumbe Wa Mkutano Mkuu Wa Vijana Taifa Ndg Emmiliana Mwasile Na Mwenyekiti Wa UVCCM Wilaya Ya Sumbawanga Mjini Ndg Joel Chalanda. 

Leo Wamefanya Ziara Ktk Kata Ya Msua Iliyopo Wilayani Sumbawanga Mjini Pamoja Na Mjumbe Wa Kamati Ya Utekelezaji Mkoa Ndg Buttoh Lubusi Na Katibu Wa Vijana Wa Wilaya Ya Sumbawanga Mjini Ndg Anthony Michael 

Katika Ziara Hiyo Mwenyekiti Wa Vijana Wa Mkoa Huo Ndugu Ramadhani Shabani Alikwenda Kutekeleza Ahadi Zake Alizozitoa Ktk Kata Hiyo Ambapo Leo Hii Ametoa Mipira Miwili Na Filimbi Dozen Moja Kwa Team Za Mpira Za Kata Hiyo.Lakini Kama Haitoshi Mwenyekiti Wa Vijana Wa Mkoa Wa Rukwa  Leo Hii Amegawa Kadi 104 Ktk Kata Hiyo.

Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Ktk Kata Hiyo  Ametumia Fursa Hiyo Kuwahasa Viongozi Wa Chama Cha Mapinduzi Ktk Mkoa Huo Kuacha Kufanya Kazi Kwa Mazoea Na Kuwataka Kwa Umoja Wao Kujitahidi Kuwafikia Wapiga Kura Mapema Na kusikiliza Kero Zao Na Kuzitatua Kwa Wakati Na Kuacha Tabia Za Kusubiri Nyakati Za Chaguzi Ndio Waanze Kushuka Kwa Wapiga Kura.

Ni Bora Wao Jumuiya Ya Vijana Waonekane Wanakurupuka Lakini Hawataacha Kushuka Mapema Na Kuyafikia Makundi Ya Vijana Mapema Na Kuyasikiliza.

Lakini Pia Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Amewataka Viongozi Wa Jumuiya Ya Vijana Ngazi Ya Kata Kushughulika Na Kero Za Vijana Na Kuakikisha Wanaingiza Agenda Za Vijana Ktk Vikao Vya Kamati Ya Siasa.Huku Akisisitiza Anayeona Anashindwa Kufanya Hivyo Basi Awapishe Wengine Wenye Uwezo Huo.


Mwisho Mwenyekiti Huyo Amewataka Viongozi Wa Jumuiya Hiyo Ya Vijana Kuhakikisha Wanawaimiza Wenyeviti Wa Mitaa Na Vijiji Wanaotokana Na CCM Kuwasomea Mapato Na Matumizi Wananchi Wao Mapema Kabla Ya Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Wa Mwaka 2019 Huku Akisisitiza Hataki Hiyo Iwe Agenda Tena Ambayo Itakinyima Chama Hicho Ushindi Ktk Uchaguzi Huo Wa Serikali Za Vijiji,Vitongoji Na Mitaa.

Mwenyekiti Huyo Pia Amewasihi Vijana Kujitunza Na Kujitambua Na Kuacha Kutumika Vibaya Kama Makalai Huku Akiwasisitiza Pia Kujiheshimu Na Kuacha Tabia Ya Kuidharirisha Jumuiya Hiyo Kwa Kufanya Matukio Ya Ovyo Kwani Hayatavumilika Ktk Uongozi Wake Na Hayana Nafasi Kabisa.Mwenyekiti Huyo Ameendelea Kuwasisitiza Vijana Wenzie Wa Mkoa Huo Kucha Kazi.


Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Pia Kesho Anatarajiwa Kwenda Kuzungumza Na Kufungua Tawi Ktk Chuo Cha Uuguzi Ktk Kata Ya Mazwi Wilayani Sumbawanga Mjini,Lakini Pia Jumapili Mwenyekiti Huyo Pia Anatarajia Kwenda Kufunga Ligi Ya Mpira Wa Miguu Iliyokuwa Inaendelea Ktk Kata Ya Malangali Wilayani Sumbawanga Mjini Iliyokuwa Chini Ya Usimamizi Wa Jumuiya Hiyo Ya Vijana.

Imetolewa Na:-

Idara Ya Uhamasishaji Na Chipukizi Mkoa Wa Rukwa

Maoni