MWENYEKITI UVCCM MKOA WA RUKWA NDUGU RAMADHANI SHABANI AFUNGUA TAWI LA CHUO CHA UGANGA SUMBAWANGA MJINI,AVUNA 95 WAPYA LAKINI PIA AMEKABIDHI MPIRA MMOJA WA BASKETBALL

Mwenyekiti Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Ndugu Ramadhani Shabani Hapo Siku Ya Jana Amefanya Ziara Ktk Chuo Cha Uuguzi Cha Sumbawanga Mjini Ambapo Pia Alipata Fursa Ya Kufungua Tawi La CCM Vyuo Na Vyuo Vikuu Ktk Chuo Hicho Rasmi.Ktk Ziara Hiyo Mwenyekiti Aliongozana Na Mwenyekiti Wa Vyuo Na Vyuo Vikuu Ktk Mkoa Huo Wa Rukwa Hassan Nguta,Mjumbe Wa Kamati Ya Utekelezaji Mkoa Ndugu Buttoh Lubusi Pamoja Na Katibu Hamasa Na Chipukizi Wa Mkoa Huo Wa Rukwa Ndugu Andrea Matanila

Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Akizungumza Na Vijana Wa Chuo Hicho Amewahasa Na Kuwasihi Vijana Hao Kujitambua Na Kujua Wazi Kabisa Kwamba Wamebeba Dhama Kubwa Ya Maendeleo Ya Taifa Hilo Hivyo Aliendelea Kuwasihi Wawewatulivu Na Wenye Kujichunga Na Kujiheshimu Wakati Wote,


Aliendelea Kuwasihi Vijana Hao Kujikita Ktk Kujielimisha Na Kuhakikisha Kwamba Wanaitumia Vyema Taaluma Yao Kwa Maslahi Mapana Ya Taifa Na Wananchi Wake.Lakini Pia Mwenyekiti Huyo Amewahasa Vijana Hao Kujitenga Na Ushabiki Wa Kisiasa Huku Akiwataka Kutokuunga Mkono Matendo Ya Kihaini Zidi Ya Serikali Na Haswa Jambo La Maandamano Yasiyofata Utaratibu Na Yasiyotaka Kutii Sheria.

Lakini Kama Haitoshi Mwenyekiti Huyo Aliendelea Kuwasihi Vijana Hao Kutokupoteza Muda Wao Kushabikia Upinzani Kwani Kwa Tanzania Hii Ya Sasa Hauna Nafasi Tena Kwani Watanzania Wanataka Maendeleo Kupitia Chama Cha Mapinduzi.Lakini Aliendelea Kuwasisitiza Hao Vijana Kwamba Wanaoendelea Kuungangania Upinzani Wanapoteza Muda Wao Kwani CCM Haitoki Leo Wale Kesho Madarakani Kwani Kila Siku Chama Hicho Kinazidi Kuwa Imara Zaidi Kuliko Jana,Hivyo Basi Iwapase Nanyi Vijana Wenzetu Mtumie Fursa Hii Leo Hii Kujiunga Na Chama Chetu Hapa Kwani Ndio Sehemu Sahihi Kabisa Ambayo Ninyi Vijana Wenzangu Mnapaswa Kuwepo.

Lakini Kama Haitoshi Ktk Uzinduzi Huo Wa Tawi Hilo La Vyuo Na Vyuo Vikuu Ktk Chuo Hicho Cha Uuguzi Cha Sumbawanga Mjini Wanachana Wapya Takribani 95 Walijiunga Na CCM Ambapo Pia Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Wa Mkoa Huo Wa Rukwa Baada Ya Kuona Vijana Hao Wamehamasika Zaidi Aliona Ni Vyema Tawi Hilo Likaongezewa Kadi Nyingine 90.Lakini Pia Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Alitumia Fursa Hiyo Kutoa Mpira Wa Basketball Moja Ambao Ulikuwa Unaitajika Na Vijana.

Lakini Pia Mwenyekiti Huyo Aliwapa Fursa Vijana Hao Wa Chuo Hicho Kutoa Changamoto Zao Ambapo Vijana Wa Chuo Hicho Waliomba Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Kuchukua Upungufu Wa Madaktari Wakufunzi Ktk Chuo Hicho Kama Changamoto Kuu Kabisa.Huku Pia Wakiomba Mwenyekiti Huyo Kuchukua Uchakavu Wa Majengo Ya Chuo Hicho Kama Changamoto Ya Pili Huku Mwenyekiti Huyo Wa Vijana Akiwa Tayari Kawaahidi Vijana Hao Kwamba Hizo Changamoto Zimepokelewa Na Wabunge Wa CCM Mkoa Wa Rukwa Watakabidhiwa Tayari Ya Kuwasilishwa Kwa Mamlaka Husika.

Imetolewa Na:-

Katibu Hamasa Na Chipukizi Mkoa Wa Rukwa

Andrea Matanila

Maoni