MWENYEKITI UVCCM MKOA WA TANGA AFANYA ZIARA WILAYA YA HANDENI

Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kujenga jumuiya ya vijana leo 10/03/2018 mwenyekiti uvccm mkoa wa tanga ndugu Omari Mwanga amefanya ziara wilayani handeni na kuongea na wanachama. Katika ziara hiyo mwenyekiti wa mkoani tanga amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa vijana mkoani hapa kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kuwa mwenyekiti wao amewaahidi utendaji uliotukuka. 

Awali, mwenyekiti huyo wa vijana alichukua fursa hiyo kuvunja makundi yote yaliyopo kabla ya uchaguzi na ametaka vijana kuungana kujenga jumuiya iliyo imara. 

Aidha, Mwenyekiti huyo wa vijana amewataka vijana wote kumuunga mkono mheshimiwa Rais na Mwenyekiti CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli kwa vitendo na namna bora ya kufanya hivyo ni kushiriki shughuli za kiuchumi ili kujikwamua kimaisha hatimaye kukuza uchumi wa nchi kwaujumla. 

Katika hotuba yake, mwenyekiti wa vijana mkoa wa tanga aliwasisitiza vijana kuunda vikundi, kuvisajili na kujiunga ili wapatiwe mikopo kutoka halmshauri.

Mwisho, mwenyekiti huyo wa vijana mkoani hapa alimpongeza mwenyekiti wa vijana taifa ndugu Kheri James  (MCC) kwa kazi anayofanya ya kujenga jumuiya ya vijana, uimara wake umekuwa ndio nguzo na ustawi wa jumuiya ya vijana. 
Pia mwenyekiti wa vijana mkoa tanga amempongeza mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya ama kwa hakika amejitoa kwaajili ya taifa letu. 

Imetolewa na; 
Ofisi ya Umoja wa vijana (CCM)
Mkoa wa Tanga 
10/03/2018
Handeni, Tanga.

Maoni