MWENYEKITI UVCCM RUFIJI NA MAKURUMLA WAHUDHULIA REDE CUP CHAMAZI

Na Shabani Rapwi.

Jumamosi 31 March 2018.

Leo Jumamosi 31 March 2018 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Rufiji Ndg.Juma Kwangaya na Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Makurumla Ndg. Suleimani Shabani Sukwa wamehudhuria michuano ya ligi ya Rede ya UVCCM CHAMAZI REDE CUP.

Lengo la kuja kutazama mechi hiyo ni kujifunza namna ya mechi hizo zinazochezwa na sheria zake na hatimaye kuanzisha katika maeneo yao.
Michuano hiyo inayohusisha matawi 13 ya Kata hiyo imeendelea leo katika hatua ya makundi ambapo Matawi  sita yalipambana kutafuta timu nne za kundi A zitazokwenda hatua ya robo fainali.

Timu zilizofanikiwa kuingia robo fainali kutoka katika kundi A ni Mfenesini, Kisewe, Bamia na Mbande Magengeni. 

Michuano hiyo ya kufunga hatua ya makundi kwa kundi B inatarajiwa kuendelea Jumamosi ijayo kutokana na kesho kuwa ni sikukuu ya Pasaka.

Maoni