MWENYEKITI UVCCM TAWI LA KWA MKONGO,ATOA NENO ZITO KWA VIJANA.

Na Shabani Rapwi-Chamazi, Dar es salaam

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Kwa Mkongo,Ndg.Jamali Josephat,Machi 25, 2018 amefanya mazungumzo na vijana wa kikundi cha ukimbiaji Jog (Vijana Combine Jog).

Na kuwataka vijana hao kuwa mstali wa mbele kwenye kuchangamkia frusa asa za maendeleo.

"Vijana wa kwa mkongo nataka muwe mstali wa mbele kwenye kuchangamkia frusa za maendeleo,nataka muwe mfano kwa vikundi vingine" alisema Jamali.


"Staki kuona kijana anakuwa kwenye kikundi kisicho na faida yeyote kwanza kutakuwa akuna maana ya kuwepo na kikundi kwenye tawi ili la kwa mkongo" 

"Msiwe msingi mbio tu,jana nilikuwa naongea na Katibu wangu Ndg.Said Paul ameniambia anafatilia usajiri wa kikundi, nimefurahi sana kusikia ili, ivyo niwaombe kuwa na upendo na mshikamano, msikubali kugombanishwa wala kukatishwa tamaa na watu wasio watakia mema, kumekuwa na maneno meng kwa watu kuwa kikundi chenu akina lolote wala chochote,msiwasikilize nyinyi jengeni umoja na mshikamano wenu" Alisema Jamali.Sambamba na hilo Ndg.Jamali aliwataka vijana wote wasio na kadi za Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kujiorodhesha maji yao ili wapatiwe kadi izo kwa wakati.

"Vijana wote ambao msio na kadi za Umoja wa Vijana,naomba Katibu nipate hidadi yao ili tufanye mchakato wa kadi" Alisema Jamali.

Uku vijana nao wakimpongeza Mwenyekiti huyu  kuwa bega kwa bega nae na kumtaka azidi kuendeleza ushirikiano zaidi.
Pia Ndg.Jamali alitoa shilingi Elf 10,000/ kuwachangia vijana hao na kutoa ahadi ya kununua jezi kwa wasio kuwa nazo, na kutoa agizo kwa Katibu Hamasa na Chipukizi kuwapokonya jezi wote ambao walichukua jezi kwa ajili ya kufanyanyia mazoezi badala yake, zimekuwa jezi za kubebe matofali na n.k.

Maoni