MWENYEKITI WA VIJANA KIPONZA AFANIKISHA UPATIKANAJI WA JEZI NA MPIRA KWA TIMU YA REDE

Kiponza,  Chamazi. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Kiponza Kata ya Chamazi Ndg.HAKIM MALIMBA amefanikisha upatikanaji wa jezi kwa timu ya mchezo wa rede ya Tawi hilo.

Zoezi hilo la ugawaji wa jezi hilo limefanyika leo katika uwanja wa rede wa timu hiyo uliopo Kiponza.


Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa jezi hizo Ndg.MALIMBA alisema Chama Cha Mapinduzi kinawapenda na kuwathamini vijana wa rika na jinsia zote.

"Napenda kuwaambia vijana kuwa Chama Cha Mapinduzi kinawapenda na kuwathamini vijana wa rika na jinsia zote na sio kuwapenda kwa maneno bali kwa vitendo" alisema MALIMBA na kuendelea. 

"Kwa kudhihirisha hili Mwenyekiti wenu wa Vijana nimeamua kupambana usiku na mchana na kuhakikisha tunawapatia jezi na mpira ili timu yetu ifanye vizuri kwenye michuano ya ligi ya Kata inayoendelea" alisema MALIMBA na kuendelea. 

"Natumai mtafanya vizuri na niseme tu viongozi wenu tunawapenda na kuwajali pia tupo bega kwa bega nanyinyi katika kipindi cha shida na raha" alisema MALIMBA.

mwisho Ndg. MALIMBA aliwataka vijana wa timu hiyo kujiandikisha majina yao na hatimaye kuweza kupatiwa kadi za Chama na Jumuiya ya vijana.

Maoni