MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA RUKWA NDG RAMADHANI SHABANI AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI NKASI, 59 WAJIUNGA NA CCM KATIKA ZIARA HIYO

Imetolewa Na Idara Ya Chipukizi Na Hamasa Mkoa Wa Rukwa
Mwenyekiti Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Ndugu Ramadhani Shabani Leo Tarehe 06/03/2018 amefanya ziara ya kikazi  wilayani Nkasi.

Mwenyekiti huyo wa vijana mkoani Rukwa Aliongozana Na Kamati Yake Ya Utekelezaji Pamoja Na Katibu Hamasa Na Chipukizi Mkao Pamoja Na Mwenyekiti Vyuo Na Vyuo Vukuu Mkoa Wa Rukwa Lakini Pia Mjumbe Wa Mkutano Mkuu Taifa Ndugu Emmiliana Mwasile Na Kupokelewa Na Mwenyekiti Wa Vijana Wa Wilaya  Ndugu Emmanuel Robert  Pamoja Na Mwenezi Wa Wilaya Hiyo Ndugu Justine Kiboko  Pamoja Na Mjumbe Wa Kamati Ya Siasa Ya Wilaya Ndugu Nassoro.


Lakini Pia Mwenyekiti Wa Vijana Huyo Pia Ktk Ziara Huyo Amezungumza Na Kamati Ya Siasa Ya Wilaya Hiyo Huku Pia Ambapo Amewaambia Imewapasa Watambue Nafasi Ya Wajumbe Ktk Kamati Ya Siasa Ni Sawa Na Hivyo Amewataka Kuacha Tabia Ya Kuitana Kwa Nyadhifa Zao Ktk Vikao Na Kuwataka Wote Wanapokuwa Kwenye Kamati Ya Siasa Waitane Ndugu Wajumbe Na Kuacha Kuitana Majina Ya Mhe DC Au Mhe Mbunge.Alisema Nataka Mtambue Wote Ninyi Ni Wajumbe Na So Vinginevyo Hakuna Mjumbe Mdogo Kuliko Mwenzie Ndani Ya Kamati Ya Siasa Na Hivyo Kuitaka Kamati Hiyo Kushirikiana Vyema Na Jumuiya Hiyo Ya Vijana Ngazi Ya Wilaya.

Lakini pia mwisho alisema jumuiya hiyo ya Vijana mkoa wa Rukwa imejipanga vyema kuahakikisha inashiriki vyema na kikamilifu Ktk uchaguzi ujao wa serikali za vijiji,vitongoji na mitaa hapo mwaka 2019 pamoja na ule mkuu wa mwaka 2020 na hivyo kuiomba Kamati hiyo ya Siasa kulitambua hilo.

Lakini pia mwenyekiti huyo ya Vijana mkoa wa Rukwa amezungumza na Kamati ya utekelezaji ya wilaya hiyo ya Nkasi ambapo amewataka kuchapa kazi na kujitahidi kufanya ziara za Mara kwa Mara ktk kuwafikia Vijana kwa wakati na kuwasikiliza kero zao,lakini pia ameitaka kamati hiyo ya utekelezaji kuhakikisha nayo inajisajili kama kikundi cha ujasiliamali huku akiwataka pia kuakikisha hata baraza Lao pia la wilaya wanalisajili nalo kama kikundi cha ujasiliamali huku akisema lengo lake ni kwamba anataka asilia tano zinufaishe jumuiya kwanza.

Lakini pia katika ziara hiyo mwenyekiti huyo pia alitembelea chuo cha uuguzi cha st bakitah na kuagiza ndani ya wiki moja chuo hicho kiwe kimepata tawi na hivyo kuwapa nafasi Vijana kupata fursa ya kushiriki vyema siasa za chama Chao na huku akisitiza kwamba hata vumilia viongozi wa vivu ktk jumuiya na hivyo ukiona umeshindwa kufanya kazi yakupasa kuwapisha wengine.


Maoni