MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA RUKWA AWATAKA WENYEVITI  WA VIJIJI,VITONGOJI NA MITAA KUWASOMEA WANANCHI WAO MAPATO NA MATUMIZI KABLA YA KWENDA KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Mwenyekiti Wa Vijana Mkoa Wa Rukwa Ndg.  Ramadhani Shabani Akizungumza Na Wananchi Wa Mazwi Ktk Mkutano Wa Hadhara Wa Kiserikali Wa Mhe Mbunge Wa Viti Maalum Ndg.  Bupe Nelson Mwakangata.  

Amewataka Wenyeviti Wote Wa Vijiji,Vitongoji Na Mitaa Kujiandaa Kwenda Kuwasomea Mapato Na Matumizi Wananchi Wao Kwani Chama Cha Mapinduzi Katika Mkoa Huo Na Haswa Jumuiya Hiyo Ya Vijana Haitaki Jambo Hilo Kuwa Agenda Tena Ya Wapinzani Katika  Uchaguzi Ujao Wa Vijiji,Vitongoji Na Mitaa Hapo Mwaka 2019.

Alisema Tunataka Wapinzani Wakose Hoja,Tunataka Kuwasafisha Kabisa Katika Mitaa Yetu Kwani Walipewa Nafasi Lakini Hakuna Walichofanya Zaidi Ya Kuendelea Kudidimiza Maendeleo Ya Wananchi Wetu, Sasa Ndugu Wenyeviti Kazi Kwenu Kwa Kuhakikisha Kwamba Mnawasomewa Wananchi Mapato Na Matumizi.

Mwisho  Mwenyekiti Huyo Alitumia Fursa Hiyo Kuwakumbusha Vijana Wa Wilaya Ya Sumbawanga Mjini Kujiandaa Vyema Na Kuakikisha Wanaunda Vikundi Na Kuvisajili Sambamba Na Kufungua Akaunti Tayari Kwa Kuchangamkia Fursa Ya Kupata Fursa Ya Kupata Mikopo Kupitia Mapato Ya Halmashauri Ya Wilaya Hiyo Kwani Amepokea Taarifa Kwamba Tayari Halmashauri Hiyo Imetenga Shillingi Milioni 50 Kwa Ajili Ya Mikopo Ya Vijana Alisema. 

Pia Nakuagiza Mhe Naibu Meya Fedha Ziwahi Kutoka Mapema Vijana Wapewe Mikopo Alisema Mwenyekiti Huyo Wa Vijana.


UVCCM MPYA MKOA WA RUKWA KWA MASLAHI MAPANA YA VIJANA

Tukutane Site

Imetolewa Na:-

Katibu Hamasa Na Chipukizi Mkoa Wa Rukwa

Andrea Matanila

Maoni