MWENYEKITI,MTENDAJI WA KIJIJI WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUWAKODISHIA MASHAMBA RAIA WA BURUNDI

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

KAMATI ya Ulinzi na Usalama wilayani Kakonko mkoani Kigoma inawashikilia Mwenyekiti na Mtendaji wa Kijiji cha Kikurazo pamoja na Warundi watano kwa kosa la kuwakodisha warundi mashamba zaidi ya Hekari 100 ambayo ni mali ya Kijiji hicho.

Viongozi hao na RAIA hao wa Burundi wanashililiwa baada ya oparesheni iliyofanywa na Kamati hiyo katika kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kukagua usalama wa mipaka ya Tanzania.

Akiizungumzia operesheni hiyo jana, Mkuu wa Wilaya ya kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wependa maendeleo kuwa kuna baadhi ya wananchi kutoka Burundi katika eneo la Kumuka wanakuja katika mpaka wa Tanzania katika Kijiji cha Kikurazo.

Ameongeza wanapofika kijijini hapo hukodishiwa maeneo hayo ambapo wamekuta wamelima Mihogo, Mahindi na Karanga wakati wananchi baadhi wanakosa maeneo ya kulimia.Amesema kuwa wao kama viongozi wa wilaya waliamua kufika Katika eneo hilo na kukuta kuna mshamba zaidi ya hekari 100 zinazolimwa na Warundi kwa kukodishiwa na viongozi wa Kijiji kwa Sh. 40000 hadi Sh.60,000 kwa hekari moja ilikujipatia fedha hizo.

"Baada ya kukuta hali hiyo waliamua kumkamata Mwenyekiti wa Kijiji na Mtendaji pamoja ma baadhi ya Warundi waliokuwa katika mashamba hayo na wanaendelea na mahojiano na jeshi la polisi baada ya hapo watawafikisha mahakamani," amesema.Ameongeza walipofika mpakani kuangalia usalama wa mpaka wetu wameukuta mpaka uko salama na wamefanya oparesheni na kubaini Warundi wanalima kwenye ardhi ya Tanzania.

*Na baada ya mahojiano wamekili kabisa wanalima na wamekodishiwa na viongozi nipende kuwaambia Warundi na viongozi wa vijiji wasiifanye Tanzania kama shamba la bibi, wananchi wetu na wao wanahitaji kulima na tutahakikisha hakuna Mrundi yeyote atakae vuna mazao hayo.

"Na tutahakikisha mazao hayo yanavunwa na wananchi wetu hatuko tayari kuona nchi yetu inaingia uhasama na nchi jirani kwaajili ya baadhi ya viongozi wasio waaminifu", amesema Kanali Ndagala.Aidha amewataka viongozi na wananchi wa mipakani kuacha tabia ya kuwakodishia wananchi wa Burundi mashamba kwa kuwa ni kosa kisheria na kwa watakao bainika watafikishwa mahakamani," amesisitiza.

Pia amesena oparesheni hiyo ni muendelezo wa oparesheni zingine kwakuwa suala hilo linaweza kusababisha kupelekea uvunjifu wa amani kutokana na miingiliano huo wa mipaka na kusababisha mipaka ya nchi kuibiwa na wageni.Mtendaji was Kijiji cha Kikurazo Merikiadesi Evarist amekiri ni kweli maeneo hayo yamevamiwa na Warundi na baadhi ya wananchi hawana maeneo ya kulimia.

Amesema yeye kama mtendaji wa kijiji hajahusika na suala hilo na ameaminiwa kuwa mtendaji wa kijiji hicho kwa muda wa miezi sita iliyopita, hivyo hakuwa anafahamu chochote kinachoendelea katika maeneo hayo.

Mwenyekiti was kijiji hicho Enosi Rwanika amesema baadhi ya wananchi ambao ndio wamiliki wa mashamba hayo wamekuwa wakiwakodishia raia hao kutoka Burundi.Amesema mwaka 2017 waliweka utaratibu wa Kuhakikisha wananchi wanagawiwa maeneo kwaajili ya shughuli za kilimo, baadhi walichukua na wengine hawakuweza kujitokeza.

"Ambao hawakujitokeza ndio hao wanaolalamika hawana maeneo ya kufanyia kilimo na waliochukua baaadhi yao wanawakodishia Warundi mashamba," amesem

Chanzo : MICHUZI

Maoni