RAIS MAGUFULI AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHATO MKOANI GEITA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali wa Chato waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay mara baada ya Benki hiyo kuchangia mfuko wa Elimu wa mkoa wa Geita kwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 50 kabla ya ufunguzi wa Tawi hilo la Benki.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwa kupiga makofi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji wakati msanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Chato alipokuwa akitoa burudani ya ngoma hiyo.

 Mmoja wa wacheza ngoma wa kikundi cha Ngoma za asili cha Chato akimwagiwa Rangi kabla ya kuonesha umahiri wake wa kucheza ngoma hiyo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Denmark hapa nchini Einar Hebogard Jensen wakati akielekea kwenda kufungua Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati msanii wa Msechu Bendi Peter Msechu alipokuwa akiimba mara baada ya kufungua tawi hilo la Benki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Chato mara baada ya kutoka kwenye ufunguzi wa tawi hilo la benki ya CRDB lilopo Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU.

Maoni