RC MAKONDA ATANGAZA VITA NA WANAUME WALIOTELEKEZA WATOTO DAR

 Katika Jamii tunapoona Mmomonyoka wa Maadili Hususani kwa Vijana kuanza Matumizi ya Dawa za Kulevya, Kutukana Matusi Mitandaoni tunaanza kulaumu familia, na katika kulaumu  anaeonekana Kulaumiwa Zaidi ni Mama ambae AMEACHIWA Jukumu la Kubeba Mimba, kulea na kutunza Mtoto Mzigo ambao unakuwa Mzito Kwa Yeye Kuubeba Mwenyewe Hatua ambayo Inasababisha Mwanamke kushindwa Kuhimili na kuanza Kuitwa Single Mother, Single Parents uku Baadhi ya kina Baba wakiingia Mitini na kwenda Kustarehe na Vimada. 

 RC Makonda amesema Tatizo linakuwa Kubwa zaidi pale ambapo Mama anaekuja Kubeba Ujauzito (mimba) anapokataliwa Na Muhusika na Kujaribu Kutoa Mimba, mwingine analazimika kutupa kichaga, au kufukuzwa kwao na Hatimae anakimbilia Mtaani na Kuanza kuuza Vitumbua , Ndizi , Uji , Karanga, samaki akitafuta hela ya Kutunza Mtoto na kumfanya Mama Ajute kwa Jambo Ambalo walifurahia Pamoja 
, hatua ambayo Imeongeza Maumivu na Machungu Mengi kwa Wanawake . 

 Mhe. Paul Makonda amesema Amebaini Idadi kubwa Ya Kina Mama Wanateseka kwa Kukosa Matunzo Stahiki ya Mtoto na Kumpeleka kutoa Maelekezo yafuatayo 

1. RC Makonda Ametoa Muda wa Mwezi Mmoja TU kuanzia Mwezi March Mpaka April mwaka huu kwa Wanaume WOTE waliotelekeze watoto kwa Wanawake Wanaoishi katika Mkoa wa Dar es Salaam. kuwatafuta watoto Wao na kuanza kutoa Matunzo Stahiki 

2. Endapo Agizo la kutoa Matunzo Stahiki halitafikiwa, RC Makonda atakutana na Kina Mama Wote wa Mkoa wa Dar es Salaam Wanaoteseka na Kadhia hii kuanzia Tarehe 09/04/2018 kufika ofisini kwake na Kukutana na Japo La Wanasheria Nguli na Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao watachukua Hatua za Kisheria dhidi ya wale wote watakoshindwa kutimiza Wajibu wao wa kisheria wa kutunza Watoto. 

3. RC Makonda pia ametoa Wiki nzima ya kusikiliza Malalamiko yanayohusiana Na masuala ya Malezi kwa watoto kupata Haki zao Stahiki, zoezi ambalo litaanza tarehe 26/04/2018. 


RC Makonda  amesema Endapo Wahusika Wote Watakaidi Kutekeleza Agizo hilo, Tayari Ameshajiandaa Kuwakabili kwa Kuandaa jopo la Wanasheria MAHIRI na Maafisa Ustawi wa jamii watakaoanza kuchukuwa hatua za kisheria kwa wanaume wanaokwepa majukumu yao kuanzia April 09 Mwaka huu kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Lengo likiwa ni kukomesha Tabia za Unyanyasaji wanazofanyiwa Wanawake Pindi wanapoomba au kudai fedha za matunzo kwa Watoto ambapo Wengi wao huishia Kupigwa , kutukanwa na Kunyanyaswa hatua inayohatarisha Ustawi wao na wa watoto wao. 

 Mhe Makonda Amehitimisha kwa kuwatakia HERI kina Mama Wote katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani na Kusisitiza Serikali ya Awamu ya Tano iko pamoja na katika kuhakikisha wanatatua changamoto kubwa na ndogo zinazowakabili Wanawake ili Waweze Kushiriki kikamilifu katika Kuijenga Tanzania Mpya.

Maoni