SEED trust yapokea vitabu1000 vya Malengo ya Dunia kwa wasioona .

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez (katikati) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo na Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju (wa pili kushoto) sehemu ya nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Bodi ya SEED Trust Tanzania, Mh. Stephen Mashishanga (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa SEED Trust Tanzania, Mh. Margaret Mkanga (kushoto) na Meneja Programu wa SEED Trust Tanzania, Peter Mwita (kulia).

Umoja wa Mataifa umetoa nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia vilivyochapishwa kwa herufi nundu (braille)(hizi ni herufi zilizovimbishwa na ambazo watu wasioona au wenye uoni hafifu husoma kwa kugusa na kidole) kwa taasisi ya Seed Trust Tanzania katika jitihada za kuwafikia wasioona. Kuna takribani watu milioni 39 wasioona na wenye uoni hafifu kote duniani leo; miongoni mwao takribani milioni 5.8 wako Afrika. Nchini Tanzania, kuna taarifa kwamba takribani asilimia 1.2 ya watu wenye ulemavu huu walitoa taarifa kwamba wana matatizo ya kuona.
 

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumzia kuhusu Umoja wa Mataifa kuwafikia watu wenye ulemavu katika kuhakikisha taarifa za Malengo ya Dunia zinawafikia watu wote wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo na Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju, akitoa salamu za serikali na kupongeza juhudi za Umoja wa Mataifa kuwafikia wenye ulemavu kwa kutoa nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za UN ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Mambo ya Sheria, Mh. Amon Anastazi Mpanju.Akizungumzia juhudi za UN kuwafikia wenye ulemavu, Mh. Amonalisema: “Lengo la 4 la Malengo ya Dunia linahusu elimu bora iliyo jumuishi na usawa wenye haki na kuhamasisha upatikanaji wa fursa za kujifunza za kudumu kwa wote. Lengo la 10 linahusu kuhakikisha kupungua kwa tofauti ndani na kati ya nchi nanchi. 

Lengo la 17linahusu kuimarisha njia za utekelezaji na kuhuisha ushirika duniani ili kufikia Maendeleo Endelevu. Shabaha hizi kwa namna ya pekee zinataja ulemavu kama kitu kitakachosaidia kuhakikisha ushirikishwaji na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika utekelezaji, usimamizi na tathmini ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Ujumuishwaji kwa hakika utahakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma. Kujumuishwa kwa watu wenye ulemavu kunatoa fursa kwao kushiriki na kutoa dukuduku zao pia.

Mwenyekiti wa Bodi ya SEED Trust Tanzania, Mh. Stephen Mashishanga akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya nakala 1,000 za vitabu vya taarifa za Malengo ya Dunia kwa wasioona iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Umoja wa Mataifa, Masaki jijini Dar es Salaam.

Maoni