SERIKALI YAFUNGA KIWANDA KWA SIKU 14 NA KUVITOZA FAINI YA JUMLA YA SH. MILIONI 40.8 VINGINE VITATU JIJINI DAR ES SALAAM

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SERIKALI imesitisha shughuli za uzalishaji kwenye kiwanda cha kutengeneza mifuko ya nailoni (viroba), cha TASIPA kilichoko jijini Dar es Salaam kwa siku 14 kuanzia leo Machi 7, 2018 baada ya kubainika kuwa kiwanda hicho kinahatarisha maisha ya wafanyakazi wake.

Sambamba na hilo, kiwanda hicho pia kimetozwa faini ya shilingi milioni 18 kwa kukiuka sheria ya usalama na afya mahala pa kazi. Aidha Mhe. Mavunde pia amevitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 22.8 viwanda vya Hengji Investment, ambacho pia kinatengeenza viroba (mifuko ya nailoni), na kiwanda kingine cha kutengeneneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited kwa makosa mbalimbali ya kukiuka Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini.

“Katika kukagua Sheria za usalama na afya mahala pa kazi, tumebaini kuwa mazingira ya kiwanda hiki cha TASIPA ni hatarishi mno kwa mfanyakazi kufanya kazi na tayari watu wa OSHA walikwishafika hapa na kutoa maelekezo, lakini hakuna kilichofanyika.” Alisema Mhe. Mavunde.

Naibu Waziri pia aliagiza kuwa muajiri huyo kutoa mikataba ya kazi kwa wafanyakazi wote kwa mujibu wa sheria namba 6 ya mwaka 2004 na mikataba iwe imekamilika n dani ya siku 14 na kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi ili aipitie.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nywele cha SH. Afrique Tanzania Limited leo Machi 7, 2018, wakati wa ziara yake ya kushtukiza kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi ipasavyo Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).

Kwa mujibu wa sharia ya usalama mahala pa kazi mfanyakazi huyu alipaswa kuvaa mask na gloves. hapa ni kiwanda cha TASUPA kinachotengeneza mifuko ya nailoni (viroba)

Naibu Waziri Mvunde akishuhudia ukiukwaji wa sharia ya usalama mahala pa kazi kiwanda cha TASUPA

Naibu Waziri Mvunde, (wapili kushoto), akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo, akizungumza na nmfanyakazi wa TASUPA ambaye alimkuta akifanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuchanganya masalia ya mifuko ya plastiki kiwanda cha TASUPA huku akiwa hana vifaa vya kujihami(protective gears).


Maoni