SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI 11.4 KUBORESHA WAKALA WA NDEGE ZAKE

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuboresha Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea na kukagua utekelezaji wa majukumu ya Wakala wa Ndege za Serikali ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa wa Serikali ambapo alizungumza na Menejimenti na wafanyakazi na kuwaeleza kuwa Serikali imejipanga kuboresha Wakala hiyo

Mhandisi Nditiye alisema kuwa azma ya Serikali ya Awamo ya Tano inayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali zinafanya kazi zake kwa weledi na uadilifu ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwatumikia wananchi. 

“Serikali inatambua umuhimu wa Wakala hii na ina imani kubwa nanyi katika kuhakikisha kuwa mnafanya kazi zenu za kusafirisha viongozi kwa usalama na kwa uhakika ili waweze kutimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi na tayari ina nia ya kuboresha taasisi hii”, amesema Mhandisi Nditiye.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiongea na wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Anayemsikiliza ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bwana Tito Kasambala

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bwana Richard Mayongela (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Wakala wa Ndege za Serikali

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akipanda kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali inayosafirisha viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali wakati wa ziara yake kwa Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam

Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali Mhandisi Bernard Mayila akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akifanya ukaguzi ndani ya ndege mojawapo inayosafirisha viongozi wa ngazi za juu wa Serikali wakati wa ziara yake alipotembelea Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka baada ya kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali wakati wa ziara yake kwenye Wakala hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.

Maoni