Sina wimbo uitwao Maneno - Nash Mc

Rapper Nash Mc ameandika ujumbe Kupitia mtandao wa Facebook na kufafanua haya yafuatayo.
 
"Naomba kuwapa taarifa wapenda muziki wangu, Sina wimbo uitwao MANENO. 

Nina wimbo unaoitwa MWANANGU ambao wanachanganya jina kwa kuuita MANENO na wala sio mpya kabisa. Ulitoka kimakosa bila urasmi miaka minne iliyopita.

 Usije ukadanganywa au kuambiwa tofauti na hapo. Na pia napenda kuwapa ushauri watu ambao wanamiliki tovuti na blogs kuwapigia wasanii husika kupata taarifa za kazi zao kabla hawajaziweka mitandaoni.

 Asanteni"

Maoni