TGNP Mtandao wakutanisha madiwani 20 kujadili kushirikiana

Zaidi ya madiwani 20, kutoka mikoa mitano na wilaya Nane wamekutana jijini Dar Es Salaam, kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Madiwani hao ni kutoka Halmashauri za wilaya za Kishapu (Shinyanga), Tarime (Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).

Madiwani hao ambao walikutana katika ofisi za TGNP Mtandao, zilizopo Mabibo Dar Es Salaam, pia walipata nafasi ya kutembelea Kipunguni na kujionea mradi unaotekelezwa katika eneo hilo.

Pamoja na kujifunza masuala mbalimbali, Madiwani hao walipata fursa ya kushirikisha masuala ya kijinsia ambayo bajeti za Halmashauri zao zimezingatia na jinsi walivyofanikiwa kutenga rasilimali za kuhakikisha bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.

Wakiwa kata ya Kipunguni iliyopo manispaa ya Ilala madiwani hao walikutana na Diwani wa Kata hiyo na kujifunza jinsi ambavyo wananchi waliopo katika Kituo cha Taarifa na Maarifa walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa kushirikiana na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji.Eneo hilo maarufu kwa wakazi wa kutoka mikoa ya kaskazini ambako yapo makabila yanayofanya ukeketaji nalo limekumbwa na tatizo hilo.

Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba akifafanua jambo wakati akiendesha mjadala kwa Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga, Ngoromole Abdul akibadilishana uzoefu na madiwani wenzake wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

Maoni