UMOJA WA VIJANA WA CCM MKOA WA IRINGA, soma zaidi

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Wa Iringa Ndg. KENANI KIHONGOSI, leo ameongoza kikao chake cha kwanza cha KAMATI YA UTEKELEZAJI UVCCM MKOA WA IRINGA. 

Kikao hicho kiliudhuriwa na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa kupitia Mkoa wa Iringa Ndg. James Mgego, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa Ndg. Zawadi A. Abdallah, Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Iringa Ndg. Abed Mhogole, Katibu Hamasa na Chipukizi Mkoa Ndg. Sufian Omari pamoja na Wajumbe wawili wa Kamati ya Utekelezaji Mkoa Ndg. Fred Chalamila na Fred Ndanzi wajumbe wanne walitoa udhuru kutokana na changamoto zilizo nje ya uwezo wao.

Katika kikao hicho, wajumbe waliweza kujadili namna ya kuimarisha Jumuiya kiuchumi, kuendeleza miradi iliyopo na kutafuta miradi mipya ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Aidha, Kamati ya utekelezaji imeridhia kuanzishwa kwa Kamati ya Mafunzo na Ulinzi ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao;-

> Mwenyekiti komredi Mussa Salum Mbungu

> Makamu Mwenyekiti komredi Ridhiwani Mfaume Ngole

> Katibu komredi Danny William Mkonda 

> Katibu Msaidizi komredi Rajan Ally Mgidange
(Wajumbe Wengine watatajwa)

Katika kikao hicho wajumbe wameridhia uundwaji wa kamati nyingine ambazo zitatangazwa baadae kutokana na umuhimu wake.

Sambamba na hilo Mwenyekiti Ndg. KENANI KIHONGOSI ametoa onyo kali kwa wote wenye nia ovu ya  kuhujumu Jumuiya ya Vijana Mkoani Iringa, Amesema hatua kali za kinidhamu kupitia kanuni ya jumuiya ya Vijana zitachukuliwa dhidi yao bila huruma.

Alimalizia kwa kuwaomba Vijana wote wanaokipigania Chama Cha Mapinduzi Mkoani Iringa wapeleke CV zao katika Ofisi za UVCCM Wilaya husika ili kuweze kuwa na database ya mkoa ambayo  ataipeleka makao makuu ya jumuiya hiyo ili Vijana waweze kutambulika na kuweza kutumiwa katika majukumu mbali mbali ndani ya Chama .

Pia Kamati ya Utekelezaji imebariki ziara ya Mjumbe wa Baraza kuu kupitia Mkoa wa Iringa Ndg. Zawadi Abdallah kutembelea Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa na kukutana na wakurugenzi ili kujua utekelezaji wa asilimia Tano kwa Vijana  na namna bora ya kuboresha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

Pamoja na hayo  Mwenyekiti amepongeza kazi kubwa inayofanywa na chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa kwa kuendelea kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo jambo ambalo linaleta imani kubwa kwa wananchi.

Mwisho mwenyekiti amesisitiza kumuunga mkono Komred Kheri James katika kutekeleza majukumu ya Jumuiya yetu pia kuwaombea Viongozi wetu wakuu wa chama na Seriikali chini ya jemedari wetu DR JOHN POMBE MAGUFULI.

Imetolewa na:-
Sufian Omary 
Katibu Hamasa na Chipukizi Mkoa wa Iringa.

Maoni