UVCCM CHAMAZI YASHIRIKI USAFI NA BONANZA KATA YA MWANDEGE

Jumapili 11 March 2018.

Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Kata ya Chamazi kwa kushirikiana na Kata ya Mwandege wamefanya usafi uliofuatia na bonanza la mchezo wa rede Katika Kata ya Mwandege iliyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Viongozi wa UVCCM Kata ya Chamazi walioshiriki zoezi hilo lililofanyika jana Jumamosi 10 March 2018 ni Mwenyekiti Ndg. NASRI MKALIPA, Katibu Ndg. JUMA BEGA ZONZO, Katibu Hamasa na Chipukizi Ndg. NAJIM NURDIN NYANZA, Wajumbe wa kamati ya utekelezaji Ndg. SALEH SELEMANI MSONGA na ASHA KUSAGA MANYAMA, Katibu wa Tawi la Kisewe Ndg. JENIPHER KUSAGA MANYAMA, Katibu Hamasa na Chipukizi Tawi la Mwembe Bamia MARIAM MUKI, Katibu Hamasa na Chipukizi Tawi la Kwa Mkongo Ndg. SHABAN RAPWI, Katibu Hamasa na Chipukizi Tawi la Kisewe Ndg. KHALFAN NJOGOLO, Mjumbe wa Mkutano Mkuu Kata kutoka Tawi la Kisewe Ndg. HALIMA MPANDA na Mjumbe kutoka Tawi la Mzambarauni Ndg. ESTER DAVID.

Mgeni rasmi katika zoezi hilo alikuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mkuranga Maarufu kama DOGO MAMBO. 

Usafi huo ulifanyika katika eneo la Kipara mwisho wa msitu panapojengwa shule ya msingi na sekondari.

Baada ya kumaliza kufanya usafi huo kulifatiwa na bonanza kubwa la mchezo wa rede ambapo viongozi kadhaa wa UVCCM Kata ya Chamazi walishiriki kucheza mchezo huo.

.
Imetolewa na
NAJIM NYANZA
Katibu Hamasa na Chipukizi
Kata ya Chamazi. 

Maoni