UVCCM CHAMAZI YATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA UMOJA WA VIJANA WILAYA YA TEMEKE NA WAKUFUNZI.

Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Chamazi jana  Jumatatu wamemaliza mafunzo ya siku tatu ya uongozi.

Mafunzo hayo yaliyoanza kutolewa siku ya Ijumaa 2 March na kuisha jana Jumatatu 5 March yalifanyika katika Chuo Cha Mwalimu Nyerere Kigamboni.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Makamu Mwenyekiti CCM Bara Taifa Ndg. Philip Mangula na kufungwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndg. Kheri James.

Viongozi wa UVCCM Chamazi waliohudhulia mafunzo hayo ni Mwenyekiti Ndg. Nasri Mkalipa, Katibu Ndg. Juma Bega Zonzo, Katibu Hamasa na Chipukizi Ndg. Najim Nyanza na wajumbe wa kamati ya utekelezaji Ndg. Asha Kusaga, Saleh Msonga na George Madaraka.


Mafunzo yalikuwa mazuri na tumejifunza sana na kutufanya kuwa na uelewa mpana wa masuala ya kisiasa hususan chama chetu cha Mapinduzi. Pia UVCCM kata ya chamazi inatoa shukrani zake za dhati kwa umoja wa vijana wa wilaya ya Temeke kwa kata zote kwa ushirikiano na upendo mkubwa kwa Muda wote tuliokuwa kambini vilevike tunatoa shukrani za dhati kwa wakufunzi wote waliotoa mafunzo hayo kwa Muda wote wa siku tatu.


Imetolewa na
Najim Nyanza
Katibu Hamasa na Chipukizi.
Kata ya Chamazi.

Maoni