UVCCM KIGOMA WAMLILIA KABOROU


Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoani Kigoma umepokea kwa masikitiko na huzuni taarifa za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa Kigoma Dk Walid Amani Kaborou aliyefariki usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam. 

Katika salamu za rambirambi toka Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Kigoma Sylivia Sigula kwenda kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa kigoma Ammandus Nzamba , UVCCM wameelezea kusikitishwa kwao na kifo cha kiongozi huyo mkoani humo. 

Sylivia amemuomba Mwenyekiti wa ccm mkoa kigoma awafikishie salamu zao za zarambirambi na mkono wa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu na jamaa na kuwataka wawe na moyo wa subira na ustahamilivi kwa wakati huu

Aidha Mwenyekiti huyo wa UVCCM amemtaja marehemu Dk kabourou katika maisha yake amekuwa kiongozi aliyetawaliwa na busara, hekima, maarifa mapana na mwenye upeo mkubwa katika medani za siasa na historia ambapo mara zote amekuwa zaidi ya mwalimu kwa vijana.

"Chama chetu kimepoteza kiongozi wake bora, msikivu na mjuzi katika masuala ya siasa na maendeleo ya demokrasia .Tunamuomba mungu mtukufu ampokee, amsaheme dhambi zake na amuweka mahali pema peponi"Alieleza Sylivia kwenye tanzia yake kwenda kwa Mwenyeliti wa CCM Mkoa Kigoma .

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa UVCCM amesema jumuia yake mkoani humo itaendelea kujifunza mambo yote mema na mazuri yaliokuwa yakifanywa na Dk Kabourou wakati wa uhai wake na jinsi alivyokuwa mahiri katika kujenga hoja na kujibu mapigo ya kisiasa . 

Sylivia ameeleza mwili wa marehemu Dr. Walid Kabourou utasafirishwa kutoka dar es salaam kuelekea kigoma kesho saa nne asubuhi. Mazishi yamategemewa kufanyika Tarehe 9 Machi 2018, siku ya Ijumaa, katika msafa wa makaburi ya Kipampa shule ya ujiji. Mwenyekiti anawaomba wanakigoma na wanaccm kwa ujumla tushiriki kwa pamoja katika kumpumzisha mzee wetu katika nyumba yake ya milele. Msiba utakua nyumbani kwa marehemu huko Bagwe, Kigoma Mjini.

Inna lilahi wa Inna Ileiyhi Rajiun .
Imetolewa na,
Mwenyekit wa vijana mkoa wa kigoma.

Maoni