UVCCM MIBURANI CUP 2018 YAANZA KWA KISHINDO

Mashindano ya Uvccm Miburani Cup 2018 yameanza rasmi  kutimua vumbi wikiendi hii kwa  michezo miwili mmoja ukiwa wa football uku mwingine ukiwa wa rede. 

 Kwa upande wa rede timu ya KEKO MACHUNGWA B imekubari kipigo cha bao 1-0 toka kwa ndugu zao wa KEKO MACHUNGWA A.

Na kwa upande wa football timu ya KEKO MACHUNGWA A imeichapa timu ya KEKO JUU bao 2-1.


 Katibu wa  Uvccm kata ya Miburani Ndg. Swaum Cholloh ambaye ndie mwanzilishi wa mashindano hayo, amewataka vijana kujituma ili kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji bora.

"Tumeanzisha Mashindano haya lengo kubwa kuona vipaji vilivyopo katika kata yetu hii,  ivyo niwaombe muyatumie vizuri Mashindano haya kuonesha uwezo wenu ili muwe wachezaji bora na wakulipwa kama Samatta na n.k" Alisema Swaum Chollah.
Wananchi wame mpongeza Katibu huyo kwa kuanzisha mashindano hayo,kwani itasaidia vijana wengi kujiepusha kufanya vitendo vya kiarifu na  kukaa vijiweni na badala yake sasa watajikita zaidi kwenye michezo.


Uku vijana nao wamwakikishia Katibu huyo amani na upendo itakuwa ni moja ya sehemu ya mashindano hayo na wamesema hawako tayali kuona mtu anavunja usalama ama amani kwenye kata yao.

Maoni