UVCCM TANGA WAZINDUA KITUO CHA ELIMU


Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Tanga chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Omar A.S Ayoub Umezindua rasmi kituo cha Elimu (Patriotic Education Center) ambacho kiko chini ya jumuiya hiyo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mtahiki Meya wa Jiji la Tanga Ndg. Selebos Mhina, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Ndg. Omari Mwanga, Katibu wa UVCCM Mkoa Ndg Zawadi Nyambo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Ya Wilaya ya Tanga Ndg. Mbarouk Asilia, Mwenyekiti na Katibu wa Senet idara ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Tanga, wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya Mwl. Twali Mshare na Mwl. Adinan Livamba na Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mnyanjani Ndg. Hemed Jenzi. 

Katika ufunguzi huo wa kituo hicho Meya wa Jiji la Tanga amechangia Shilingi Laki tano (500,000) ili kusaidia uendeshwaji wa Shuhuli za kituo hicho.

Kituo hicho ambacho kimesajili wanafunzi 170 ambao miongoni mwao ni wanafunzi wanaorudia Mitihani ya kidato cha nne na cha sita pamoja na QT kitatoa Elimu hiyo bure bila malipo yeyote ili kuwasaidia Vijana walio kwenye mkwamo wa kielimu kuweza kufikia ndoto zao.

Katika Hafla hiyo pia UVCCM wilaya ya Tanga imewakaribisha wanachama wapya 31.

Imetolewa na Ofisi ya UVCCM Wilaya ya Tanga.

Maoni