UVCCM WILAYA YA LUDEWA WAWAFARIJI CHIEF KIDULILE SEKONDARI KWAAJALI YA MOTO

 Umoja wa vijana wilaya ya ludewa umeonekana kusikitishwa na tukio la kuungua moto bweni la kidato cha sita shule ya secondary Chief kidulile, moto huo ambao uliibuka na kuzua taharuki shuleni hapo majira ya jion kukiwa na kiza. 

UVCCM chini ya mwkt wake theopester Mhagama na katibu wake Hassan kapolo,wameonekana kusikitishwa Sana na tukio hilo kwani sote tunajua madhara yatokanayo na moto. 

Ambapo katika ajali hiyo kumeweza kutokea madhara makubwa kwa wanafunzi kuunguliwa vifaa vyao vya masomo na Nguo, magodoro na mashuka na kusababisha kukosa huduma za kisingi kwa wanafunzi hao na kwa bahati nzuri Hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa wala kupoteza Maisha. 


UVCCM kupitia viongozi wao wameonekana kupaza sauti kwa wadau mbalimbali kuweza kusaidia mahitaji ya msingi kwa vijana Hao kwani Wanahitaji mahitaji ya msingi ili kuweza Kukaa sawa baada ya tukio hilo. Akiongea kwa njia ya simu katibu wa uvccm wa wilaya hiyo hassan kaporo ameweza kubainisha mahitaji yanayohitajika ni kama vile Nguo, magodoro, mashuka, mafuta ya  kupakaa, daftari, peni, blanket na ukarabati wa Jengo lenyewe.
 
Wameweza kubainisha kuwa wameamua kutumia mbinu shirikishi kwa kuchangisha michango kwa wadau mbalimbali ili kuweza kufanikisha zoezi hilo Mratibu wa zoezi hilo la kusaidia vijana hao ni mwkt wa uvccm wa wilaya hiyo ndugu theopester mhagama unaweza kuwasiliana naye nakuweza kufikisha mchango wako. 


Shukraani kwa wadau ambao wameweza kuguswa na kuchangia, pongez kwa familia ya fillikunjombe kwa michango yao hakika wanarudewa wanafarijika kuona bado tupo pamoja. 
Aidha viongozi hao wameonekana kuwaomba watu kusaidia hilo na kuacha itikadi za kisiasa kwani majanga ni hatari kwa maisha yetu kwa hiyo ni lazima tuwajibike.

Chama Cha mapinduzi tunawapa Pole kwa janga hili la moto.

Imetolewa na Tithok Stambuli Mtokoma na Erasto k kizumbe kutoka ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe.

Maoni