UVCCM WILAYA YA RUFIJI IMEFANYA KAMATI YA UTEKEREZAJI

Umoja wa vijana wilaya ya Rufiji, mefanya kamati ya utekerezaji chini ya Mwenyekiti Uvccm (W) Rufiji Ndg. Juma kwangaya na Katibu wa Umoja wa vijana wilaya ya Rufiji Ndg Simba M Simba

Kamati ya utekerezaji iliyo kaliwa tarehe 29/03/2018 ilikua na ajenda mbalimbali ya kujenga Uvccm Rufiji na kuwa Mpya yenye kuvutiwa na kijana yeyote.

Sambamba na ajenda hiyo pia Uvccm Rufiji imewataka vijana kuacha kutumika katika maandamano yasiyo na tija na badala yake wajikiti katika kuimarisha uchumi ili kuikomboa Taifa letu la Tanzania.
Pia Uvccm Rufiji imempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa DR JOHN POMBE JOSEPH MAGUFURI kwa kazi nzuri anayoifanya ambayo inapelekea Tanzania yetu kuwa miongoni mwa Nchi ambazo Uchumi wake Unakua kwa kasi.

Pia Uvccm Rufiji inampongeza Mwenyekiti Uvccm Taifa Ndg Kheri James kwa kurudisha imani kwa Vijana kuwa Ccm ndio kimbilio la kila kijana.
 
Imetolewa na 
Juma s Kwangaya
Mwenyekiti Uvccm (W) Rufiji

Maoni