UWT WILAYA YA NJOMBE WASEMA TUNASHUGHULIKA NA KERO ZA WANANCHI, HATUHANGAIKI NA WAPINZANI. 

Tumethubutu na tumeweza, Haya ndio maneno mazito ambayo yamesikika vinywani mwa viongozi wa Jumuiya hiyo wilaya ya Njombe chini ya Mwenyekiti  wake Bi. Angela Mwageni na Katibu wake Bi. Grace Haule, wameonekana kutembea kifua mbele kwa kushirikiana na jamii nzima hasa kupitia Jumuiya yao kwa kufanya shughuli za kijamii, Kama vile kuwalipia watoto wanaoishi  mazingira magumu, kuhamasisha wanawake kujishughulisha na shughuli za uchumi hasa kilimo na ufugaji na kuanzisha SACCOS katika Kata mbalimbali, na kuwajengea uwezo wa kukopa fedha katika halmashauri husika .
Katibu wa Jumuiya hiyo ameonekana kutukuka katika kusimamia kile ambacho wamepanga ndani ya Jumuiya  hiyo .

Wameonekana kumduwaza Mwenyekiti  wa UWT Taifa  Bi. Gaudensia Kabaka kwa kushuhudia hayo na kumwacha akiwasifu wanawake hao. 

Wamesema wao hawana sababu ya kuhangaika na kupambana na wapinzani upinzani utapotea wenyewe kwasababu wao wanapambana na ccm, sisi tunashughulika kero za wananchi.,kwani tunaamini tukifanya hayo jamii nzima itatuunga mkono juhudi za ccm.

Viongozi hao Wameonekana kutembea kifua mbele kwani wanapewa ushirikiano mkubwa na wanawake bila kujali itikadi za vyama vyao na kujikuta wakipenda namna ya kasi ya utendaji wa jumuiya Hugo. kwakuwa wamekuwa msaada sana katika kupambana na changamoto za jamii nzima. 

Kwakuthamini mchango wa jumuiya hiyo wanawake  wameonekana kujiunga na umoja wa wanawake ccm ilikuweza kuhakikisha wanaupa nguvu umoja na kuwa mwiba kwa watu wanaobeza jitihada za ccm.

Afisa mipango wa jumuiya Hiyo Bi Grace Haule amesema wanawake Njooni ccm -uwt muone mambo yanavyoenda na roho zenu ziweze kutulia, Huku mwkt wake akiwapasha na kusema upinzani usahau ccm imebadilika tukipanda jukwaani ni kuwaonesha wapiga kura nini tumefanya haina sababu ya kufanya vurugu wakati wa kuomba kura. 
Hakika mtandao wa habari kutoka ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe tunawapongeza sana ndugu zetu. 

Imepewa Nguvu na siasa na uenezi mkoa wa Njombe,imetolewa na Titho stambuli Mtokoma na Erasto kizumbe

Maoni