VILABU LIGI KUU VYASHAURIWA KUWEKEZA KWA KUWA NA TIMU ZA WACHEZAJI WA UNDER 20



Na Agnes Francis,Globu ya jamii

VILABU vya soka vinavyoshiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara vimeshauriwa kuhakikisha wanawekeza kwenye timu za wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (Under 20). 

Kwani kuna umuhimu mkubwa kwa vilabu hivyo kuwekeza kwa wachezaji wenye umri huo.Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga ambapo amesisitiza ni muhimu kwa vilabu kuwa na timu za Under 20.

Ameipongeza timu ya Mbao ambayo imeonesha kuwekeza katika Academy ya vijana wanasoka under 20 na amewataka timu zingine kuiga mfano huo."Naipongeza timu ya Mbao kwa kuwa na utamaduni wa kuhakikisha timu ya wachezaji wenye chini ya miaka 20 wanaisimamia vema.

" Mbao kwenye mechi zao nyingi wanatembea na wachezaji wao wa Under 20 na kwenye mechi za kirafiki wamekuwa wakiwatumia na lengo nikuwajengea uwezo na uzoefu mapema,"amesema Jaffary Idd Maganga.Ameongeza wakati Mbao inawekeza kwa wachezaji vijana kwa vitendo,vilabu vingine bado havijaamua kuandaa wachezaji kupitia wachezaji wenye umri mdogo walionao.

Amefafanua vilabu vingi wanaandaa timu za Under 20 pindi wanapoona kuna mashindano mbeleni ndio utaona wanaandaa vijana."Na hili si jambo Zuri, tuwe na utamaduni wa kuanzisha Academy katika vilabu vyetu," amesisitiza Jaffary. 

Amesema timu yao imefanikiwa kutoa wacheza watano kuungana na kikosi cha Timu ya Taifa vijana chini ya umri wa miaka 20 (Under 20). "Mwalimu wa kikosi cha Timu ya Taifa chini ya Umri miaka 20 (under20) Salum Mayanja ameona uwezo wa vijana wetu walivyo na uwezo wa hali ya juu mpaka imemfanya kuita vijana 5 kutoka kwenye Academy yetu kujiunga na kikosi hicho.

"Vijana hao ni Rajab Odasi, Paulo Peter, Mohammed Mussa, Osca Masai pamoja na Lusajo Mwaikenda,"amesema Jaffary.

Maoni