WANANCHI TABORA WAJITOKEZA KWA WINGI USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeendelea na zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa mkoa wa Tabora, ambapo Wilaya zote zinaendelea na zoezi hilo. 

Akizungumzia mwenendo wa zoezi hilo Afisa Usajili Mkoa wa Tabora Bi Grace Msaky, amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa na kwamba wananchi wameelewa umuhimu wa Vitambulisho.

Amesema; kuhakikisha wananchi wanapata huduma na wanafikiwa mahali walipo kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa sasa zoezi wanaendesha kwenye Vijiji na Mitaa wanakokaa wananchi na kwamba wananchi wanajulishwa muda na wakati wa kufika kwenye vituo kupata huduma hiyo.

“ kwa sasa wananchi wanaelewa utaratibu; ila changamoto ni baadhi ya wananchi kufika siku za mwisho wa zoezi na kufanya zoezi kuchukua muda mrefu kwenye baadhi ya Kata kinyume na ratiba iliyopangwa” alisisitiza.Mbali na Tobora mikoa mingine 19 inaendelea na zoezi kwa Tanzania Bara huku Tanzania Zanzibar zoezi hilo likiwa limekamilika kwa asilimia 99%. 

Wananchi wa kata ya Ipuli mtaa wa Ipuli Halmashauri ya Wilaya ya Tabora wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye mashine maalumu za uchukuaji taarifa muhimu za Usajili zikiwemo upigaji picha, alama za vidole na saini ya kielektroniki.

Mkazi wa Mtaa wa Ipuli Bi Halima Abed akiwa kwenye zoezi la kupigwa pichwa ilikukamilisha Usajili

Bi Maimuna Shabani Bundala Mkazi wa mtaa wa Ipuli akiweka saini ya kielektroniki kwenye mashiya ya Usajili wakati zoezi hilo likiendelea kwenye mtaa wake.

Bw. Shaban Yasin wa Kata ya Ipuli Mtaa wa Nane Nane akichukuliwa alama za Vidole kwenye zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.

Maoni