WATANZANIA TUDUMISHE TUNU ZETU ZA AMANI,UMOJA NA MSHIKAMANO KATIKA KIPINDI HICHI CHA SIKUKUU ZA PASAKA:-MWENYEKITI UVCCM RUKWA

"Ndg. Watanzania Nitumie Nafasi Hii Ya Uzima Na Afya Tele Kumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa Kila Jambo Anitendealo Katika Maisha Yangu Lakini Pia Niungane Na Wakristo Wote Duniani Katika Kusherekea  Sikukuu Ya Kufa Na Kufufuka Kwa  Yesu Kristo  Miaka2000 Iliyopita. Ndugu Watanzania 
Tutumie Sikukuu Hii Katika Kudumisha Mambo Yafuatayo"

"Tuungane Kwa Pamoja Na Watu Wote Wenye Uhitaji Maalum Kama Vile Masikini, Walemavu, Wagonjwa Na Wasiojiweza Ikiwa Ni Njia Pekee Ya Kuwafariji Ndugu Zetu Hao"

Lakini Pia Tuungane Kwa Pamoja Katika Maombi Na Sala Zetu Kwaajili Ya Amani,Umoja Na Mshikamano Wa Taifa Letu Tanzania.

Lakini Kama Haitoshi Tuzidi Kumuombee Mhe Rais Wetu Mpendwa Dkt  John Pombe Magufuli  Kwa Kazi Kubwa Ambayo Anaifanya Ikiwa Imebeba Maslahi Mapana Ya Taifa Letu,Kazi Kubwa Hiyo Aifanyayo Imejawa Na Chuki, Vita Na Kila Aina Ya Mapambano Yanayofanywa Na Watu Wasiopenda Kuiona Tanzania Mpya Yenye Neema Na Matumaini Mapya Kwa Wanyonge.

Tunapo Kumbuka Kufa Na Kufufuka Kwa Yesu Kristo  Tunakumbushwa Kwamba Sababu Kubwa  Ya Kifo Chake Ni Usaliti Uliofanywa Na Mwanafunzi Wake Yuda Iskariyote  Ambaye Alipewa Vipande Thelathini Vya Fedha, Hivyo Basi Nasi Kwa Pamoja Tuungane Kuwakemea Wazi Wazi Bila Ya Kuwaonea Aibu Vibaraka Wote Wa Mabeberu Ambao Wanajaribu Kutaka Kulisaliti Taifa Letu Sababu Ya Njaa Na Tamaa Yao Ya Fedha Na Madaraka.

Lakini Pia Nitumie Fursa Hii Kuwaomba Viongozi Wetu Wa Dini Katika Kipindi Hichi Cha Sikukuu Hii Ya Pasaka Kuhubiri Somo Linalolenga Daima Kuwaunganisha Watanzania Kuwa Wamoja Na Wenye Mshikamano.Niwaombe Viongozi Wetu Wa Dini Mtusaidie Watanzania Kukemea Mbegu Ya Ufitini Na Mgawanyo Wa Tanzania  Ambayo Imeanza Kupandwa Na Wapinzani Wa Serikali Ya Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Mwisho Niwatakieni Sikukuu Njema Wakristo Wote Wanaosheherekea Sikukuu Hii Ya Kufa na Kufufuka Kwa Yesu Kristo.

Ndugu Watanzania Tukumbuke Amani,Umoja Na Mshikamano Wa Taifa Letu Ni Muhimu Na Ni Tunu Kwa Taifa Letu Daima Tuzienzi Tusikubari Kuzipoteza.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Imetolewa Na:-

Ramadhani Shabani

Mwenyekiti UVCCM Mkoa Wa Rukwa. 

Maoni