WATU 11 WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA.

Mahakama moja India imewahukumu kifungo cha maisha jela watu 11 kwa kumuua muuzaji nyama Muislamu kwa jila la Alimuddin Ansari, Juni 2017, waliemshuku kwa kusafirisha nyama ya ng'ombe.

 Ni hukumu ya kwanza kuhusiana na kile kinachofahamika kama ulinzi wa jadi wa ng'ombe. 

Limetajwa kuwa ni moja kati ya mashambulio kadhaa yanayohusiana na ng'ombe, mnyama anayeaminika kuwa nimtakatifu kwa Wahindu.

Maoni